SoC04 Hakikisha unaweza kuishi miezi sita bila mshahara na usiathirike, hapo utakuwa mstaafu mzuri ajaye

SoC04 Hakikisha unaweza kuishi miezi sita bila mshahara na usiathirike, hapo utakuwa mstaafu mzuri ajaye

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
Maisha ya ajira yanafanana na ndoa , kwenye ndoa kila siku watu watu wanatamani kuingia huko mpaka kwenda kwa waganga ila wanasahau kitu kimoja ambacho ni kujiandaa kuishi ndani ya ndoa hiyo na kwenye ajira kila siku watu hutafuta kazi ila wanasahau kuwa kuna siku wataishi bila hiyo kazi.

Unapotafuta kazi usisahau pia kuna siku utaishi bila hiyo kazi hivyo hali uliyonayo kabla ya kupata kazi inaweza kujirudia siku utapoanza kuishi bila hiyo kazi kama tu utashindwa kujiandaa vizuri.

Yawezekana pasiwe na kanuni ya kuishi maisha ya ajira ila la msingi ukifika kwenye ajira hakikisha unatengeneza tena ajira nyingine itayokupa mshahara wa ziada na ukifanikisha hilo basi utakuwa na vigezo vyote vya kuitwa mstaafu atakayefurahia mapumziko yake.

Upo kwenye ajira kwa muda gani? Je mshahara ukisimama sasa utaweza kuishi kwa muda gani bila kuingia kwenye madeni?

Jitahidi uwe na uwezo wa kuishi miezi sita bila mshahara na usiathirike na hicho ndio kipimo kikubwa kuwa umejiandaa vyema kustaafu.
 
Upvote 5
Ni mipango mibovu tu watu,poor management of funds.kwa pensions inayotolewa kila mwenzi hakuna mtumishi wa umma anaweza akashindwa juishi.
 
Mfano:mtumishi kama mwal.mwenye anayestafu kwa mshahara wa 1.3 kila mwezi anapewa karibu 350K.
Sasa kwa mtu ambaye ni msataafu hana familia anashindwaje kuishi kwa 350K??
 
Back
Top Bottom