Hakikisho la Usalama Kesho Saba Saba, Hali ni Shwari Kabisa, Usalama Umeimarishwa!, Umetolewa Mwito Tujitokeze kwa Wingi, Kilele cha Saba Saba!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi,
Hili ni Hakikisho la Kiusalama, kesho hali ni shwari kabisa, usalama umeimarishwa!, Umetolewa Mwito, Wananchi tujitokeze kwa wingi, kwenye Maonesho ya Saba Saba!.
============
Mheshimiwa rais Dr Samia [amefanikiwa] kutuletea mashine za kisasa sana... Unaona kuanzia utambuzi ukienda kwenye desk la immigration... na hatua nyingine unaenda kwenye deski ambazo zinafuata."

Waziri Katambi: "Watanzania wajitokeze kwenda kujisajili ili wapate vitambulisho vyao. Jamii namba hii ni muhimu kuwa nayo... ni sehemu mojawapo ya kuwasaidia kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na serikali."


View: https://youtu.be/YE2mEC-pYnU
Mimi Mwenyewe Nitakuwepo.
Karibuni Sana,

Paskali.
 
Binafsi sioni wa kuandamana,twendeni sabasaba salama salmini,
Labda wezi ndiyo watahuzunika sana,maana katika matukio ya aina hii kwao huwa ni fursa adimu sana!...
#So I can prove, watakao fanya maandamano kesho ni purely thieves on duties!..😀
 
well done mwalimu Paskali,

well done waziri Patrobas Katambi,

well done Dr Samia Suluhu Hassan 🔥 👊
 
Selikali wameleta taharuki ya kipumbavu sana!

Wameyapaisha haya maandamano wakati kilikuwa kitu kidogo sana, na sasa watu waliopeleka mabanda yao kule sabasaba watakula hasara sana.

Kubwa kuliko ujumbe wa maandamano umefika kirahisi mno.
Kuanzia Kamata hadi Mbagala ni wanajeshi wenye mitutu, uliona wapi?
 
Paskali bana. Umeshahau octoba hakukuwa na nywinywi wala ..... ila unajua kilichotokea. Acha watu wapumzike majumbani kwao.
 
Usalama hauwezi kuhakikishiwa na mtu. Hali ya usalama inaonekana bila kuhakikishiwa. Mambo ya kuanza kusimamishwa hovyo na kukaguliwa na kuobwa hela ya kula na polisi sisi wengine hatutaki tabu nao tutajikalia nyumbani.
 
Tatizo lako wewe una uchawa uchwara fulani hivi. Ya kesho iachie kesho yenyewe itaamua!
 
Chawa naona umeona watu hawatajitokeza kwa wingi, sasa unapiga debe. Na mwendo huu utatumika hadi kwenye mashindano ya AFCON.
 

Haji mtu huko. Huo ni mtego ili wamwage tena damu za watu. Tunajua wanataka kutoa tena sadaka za damu. Haji mtu huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…