Hakikisho la Usalama Kesho Saba Saba, Hali ni Shwari Kabisa, Usalama Umeimarishwa!, Umetolewa Mwito Tujitokeze kwa Wingi, Kilele cha Saba Saba!

Hili andiko halina maana yoyote uncle Paskali hivi leo hii mwandishi kama wewe unakosa cha kuandika?

Kimsingi ni bora ungejikita kuelezea kitu kinachoitwa maandamano chanzo chake ni nini ? Kipi kifanyike ili kuondoa hisia au kitu kinachoitwa maandamano?

Wewe ni mwandishi na unasomeka mpaka na viongozi tumia kalamu yako kuandika madhara ya haya maandamano. Nadhani unakumbuka tukio la mwaka 2011 pale Tunisia maandamano yalisababishwa na kijana mmoja tu kwa sababu ya hawa viongozi kujifanya viziwi.
 
Mkuu siku hizi una hallucinate.
Saba saba hakuna watu, thanks to Katambi & co.
 
We mwenyewe nlitegemea ntakuona hapa sjakuona mmetuacha wenyewe na miziki yetu kama tumepagawa😥😥😥 77 tumepata hasara kusafirisha vitu wateja hamjaja. Mje bas ata kesho bas tupunguze mzigo
 
Serikali imejiweka kwenye mtego mbaya kabisa.
Maana kwa sasa maandamano yakitangazwa tu askari watasambaa kama hivi Leo.
Maana yake hata askari wenyewe wanaweza wakaanzisha matangazo ya maandamano kwenye mitandao ili wapate posho au shughuli ya kufanya.
Na Serikali lazima iweke maaskari kila matangazo ya aina hiyo yakifanyika na biashara lazima zifungwe hiyo wiki kwa kuogopa kuwa inaweza kuwa kweli wakaandamana.

Kwa hiyo,makundi yote yanayonufaika na maandamano au vitisho vyake kama vile akina Shehe Mwaipopo,Askari wa aina zote nk watakuwa wanahamasisha maandamano kila wakijisikia ili wanufaike bila kutumia gharama kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…