1. hatimiliki= Hati / Nyaraka ya kutambua umiliki wako kwenye jambo fulani (ardhi nk)
2. hakimiliki= Haki ya kutambuka kuwa wewe ni mmiliki wa mali, bidhaa au jambo lolote la uvumbuzi ambaolo limehusisha uwekezaji wa muda, akili nk (kwa mfano, utunzi wa kitabu, ugiunduzi wa teknologia mpya, mbegu ni)
Kwa mujibu wa Kamusi ya TUKI
( hati* nm [i-/zi-] 1 document; memorandum; certificate. 2 deed: ~ ya kumiliki title deed. 3 handwriting, script. (Kar))
(haki* nm [i-/zi-] warrant, right, prerogative, ownership; justice: stahiki ~ be worthy, be fitting; be obligatory; ~ ya kipekee monopoly; ~ ya kupiga kura suffrage. (Kar)
Miliki: milik.i[SUP]1[/SUP]* kt [ele] 1 own, possess: Mali yote ya umma ina ~wa na serikali all public property is owned by the government. 2 reign, have authority. (tde) milikia, (tden) milikiana, (tdew)milikiwa; (tdk) milikika;(tds) milikisha. (Kar)
miliki[SUP]2[/SUP]* nm [i-/zi-] possession. (Kar)