Hakimu adaiwa kujiua akiwa 'Guest House' Sumbawanga

kuifia gesti kunazua maswli mengi zaidi.

1. kwanini alienda kulala gesti?
2. alikuwa peke yake?
3.alikunywa sumu au alinyweshwa?
4.
Ulevi wa kupindukia na uzinzi/uasharati au wivu wa kimapenzi vimekuwa ni vyanzo vikuu vya mauaji au kujiua.
Guest ni nyumba ya kulala wageni. Wapenda ngono wamegeuza maana.
Kwa mfano unaenda Mbeya, utalala kwa balozi?
 
Yes, kwanini alilala guest??

hili ni swali zuli ili kujua kama kulala guest ni utaratibu wake/ alikuwa safarini/ alitaka kuwa faragha/ alikwepa kitu flani/ ali..??
Kujiua ni kosa la jinai. Mtu huchagua sehemu nzuri bila kubughuziwa ili afanye anachotaka.
Unywe sumu halafu mtu atokee huko akuwahi akupeleke hospital upone. Unafikiri utabaki salama mbele ya mkono wa sheria? Inapofika hatua ya mtu kujiua ujue nafsi imekata tamaa. Watu wanamatatizo ukizingatia kipindi hiki cha hali ngumu
 
Ulichoandika hapa umenikumbusha wakati ninasoma Jurisprudence and Legal Theory,Lecturer alitupa swali Je Suicide ni Crime? jibu lilikuwa ni Suicide sio crime mana mtenda kosa anakuwa ameshakufa marehemu,pia kingine ili kosa liwe kosa yaani Crime lazima kuwe na sheria (statute) inayolitaja hilo kosa Actus Reus na Mens Rea yake.
Hitimisho kujiua sio jinai,ila kujaribu kujiua ndio kosa kisheria mana kanuni ya adhabu imetaja hilo kosa Rejea kifungu cha 217 Cha Kanuni ya Adhabu Sura 16 R.E 2019.
 
Sasa kwanini alienda kulala Gesti kwani hana kwake hapo sumbawanga?

Na Usikute nyumbani aliaga kasafiri kikazi.
 
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kasanga iliyopo Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Michael Royan (31) anadaiwa kujiua kwa kunywa sumu katika nyumba ya kulala wageni ya ‘gesti’ iliyopo Manispaa ya Sumbawanga mkoani humo.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumanne Novemba 29, 2022 Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Theopista Mallya amesema tukio hilo limetokea Novemba 27 mwaka huu akiwa amelala katika nyumba ya wageni.

Amesema kuwa asubuhi ya siku hiyo ofisa upelelezi wa mkoa wa Rukwa alipigiwa simu na mmiliki wa nyumba hiyo na kueleza kuwa kuna mteja ambaye amelala na hajaamka na inaonekana kuwa amepoteza fahamu.

Kamanda Mallya amesema baada ya polisi kufika eneo hilo waliingia ndani ya chumba hicho na kumchukua mtu huyo kisha kumpeleka hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Sumbawanga ambapo alipokelewa na baada ya uchunguzi wa awali wa kitabibu ilibainika kuwa mtu huyo amefariki dunia.

Amesema kuwa Polisi walipoanza uchunguzi wa tukio hilo walibaini kuwa marehemu alikua ni mtumishi wa Serikali katika idara ya mahakama mkoani hapa katika mahakama ya mwanzo na kituo chake kilikuwa ni Mahakama ya mwanzo Kasanga.

Kamanda huyo amesema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa huenda marehemu alikunywa sumu, lakini baadhi ya viungo vyake vya mwili vimechukuliwa na kupeleka sampuli kwa mkemia mkuu ili kupata majibu sahihi ya nini kilicho sababisha kifo cha Hakimu huyo.

Amesema marehemu hakuacha ujumbe wowote hivyo imekua ni vigumi kufahamu sababu za tukio hilo lakini amedai kuwa jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na litatoa taarifa baada ya uchunguzi huo kukamilika.

MWANANCHI

Viungo vyake vya mwili!!
Sasa vinahusiana nini kuondoka na viungo vya marehemu!hii nchi yetu hii bhana.
Hivi huko ma ulaya huko haya makitu yapogo?
 
idara mbili ukikoswa koswa na kupigwa kisukari,magonjwa ya ajabu basi kifo cha kujiua au kuuliwa
*hakimu
*askari
 
Yes, kwanini alilala guest??

hili ni swali zuli ili kujua kama kulala guest ni utaratibu wake/ alikuwa safarini/ alitaka kuwa faragha/ alikwepa kitu flani/ ali..??
Kuna member anadai jamaa alikuwa na demu wakapima ngoma...
 
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kasanga iliyopo Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Michael Royan (31) anadaiwa kujiua kwa kunywa sumu katika nyumba ya kulala wageni ya ‘gesti’ iliyopo Manispaa ya Sumbawanga mkoani humo.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumanne Novemba 29, 2022 Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Theopista Mallya amesema tukio hilo limetokea Novemba 27 mwaka huu akiwa amelala katika nyumba ya wageni.

Amesema kuwa asubuhi ya siku hiyo ofisa upelelezi wa mkoa wa Rukwa alipigiwa simu na mmiliki wa nyumba hiyo na kueleza kuwa kuna mteja ambaye amelala na hajaamka na inaonekana kuwa amepoteza fahamu.

Kamanda Mallya amesema baada ya polisi kufika eneo hilo waliingia ndani ya chumba hicho na kumchukua mtu huyo kisha kumpeleka hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Sumbawanga ambapo alipokelewa na baada ya uchunguzi wa awali wa kitabibu ilibainika kuwa mtu huyo amefariki dunia.

Amesema kuwa Polisi walipoanza uchunguzi wa tukio hilo walibaini kuwa marehemu alikua ni mtumishi wa Serikali katika idara ya mahakama mkoani hapa katika mahakama ya mwanzo na kituo chake kilikuwa ni Mahakama ya mwanzo Kasanga.

Kamanda huyo amesema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa huenda marehemu alikunywa sumu, lakini baadhi ya viungo vyake vya mwili vimechukuliwa na kupeleka sampuli kwa mkemia mkuu ili kupata majibu sahihi ya nini kilicho sababisha kifo cha Hakimu huyo.

Amesema marehemu hakuacha ujumbe wowote hivyo imekua ni vigumi kufahamu sababu za tukio hilo lakini amedai kuwa jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na litatoa taarifa baada ya uchunguzi huo kukamilika.

MWANANCHI
Kwanza natoa pole kwa familia ndugu na jamaa kwa msiba huu mzito.

Jambo la pili ninahisi huyuHakimu hajajiua bali kasaidiwa kufa.

Uchunguzi wa kina ufanyike.
 
Yes, kwanini alilala guest??

hili ni swali zuli ili kujua kama kulala guest ni utaratibu wake/ alikuwa safarini/ alitaka kuwa faragha/ alikwepa kitu flani/ ali..??
Mahakama anayofanyia kazi na gest ilipo ni zaidi ya kilometa 100 kwahiyo huyo alikuja mjini sumbawanga kutokea kasanga, labda hana ndugu hapo mjini
 
Back
Top Bottom