Hakimu kesi ya Mfalme Zumaridi agoma kujitoa katika kesi hiyo

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Monica Ndyekobora anayeendesha kesi ya jina inayomkabili Diana Bundala maarufu ‘Mfalme Zumaridi’ amegoma kujitoa katika kesi hiyo kwa maelezo kuwa maombi ya mshtakiwa huyo anayetaka ajitoe hayana mashiko.

Hakimu Ndyekobora ametoa uamuzi huo leo Jumatano Julai 27, 2022 huku akisisitiza kwamba kesi hiyo itaendelea kusikilizwa chini yake.

Baada ya kutoa uamuzi huo, hakimu aliitaka mahakama iendelee huku wakili wa Utetezi, Steven Kitale akisema upande huo hauoni sababu ya kuendelea na kesi hiyo na kuomba ipangiwe tarehe nyingine ili kutoa nafasi kwao kuanika sababu za kwa nini mteja wao amemtaka hakimu huyo kujiondoa katika kesi hiyo.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo, Ndyekobora ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 10,2022

Chanzo: Mwanachi
 
haki ipo wapi. Hakimu ana maslahi gani hadi ang'ang'anie kusikiliza kesi ya mtu ambaye hana imani naye
 
Mahakimu wengi huwa wanajitoa wanapokabiliwa na no confidence vote na watuhumiwa, na tuelewe kuwa anayepata side effects nyingi ni suspect ,maana itabidi atafutwe hakimu mwingine na kesi inaanza upya yaani ushahidi inabidi uanze upya, hii linaleta uchelewesho wa kesi
 
Mbona kesi zipo nyingi hapo mahakamani hakimu achukue kesi nyingine aendelee nayo hiyo amuachie hakimu mwingine.
Anang'ang'ania kitu gani?
 
Zumaridi anaonewa..hizo ni chuki binafsi..hakimu naye kalambiswa asali na watesi wa zumaridi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Monica Ndyekobora anayeendesha kesi ya jina inayomkabili Diana Bundala maarufu ‘Mfalme Zumaridi’ amegoma kujitoa katika kesi hiyo kwa maelezo kuwa maombi ya mshtakiwa huyo anayetaka ajitoe hayana mashiko.

Hakimu Ndyekobora ametoa uamuzi huo leo Jumatano Julai 27, 2022 huku akisisitiza kwamba kesi hiyo itaendelea kusikilizwa chini yake.

Baada ya kutoa uamuzi huo, hakimu aliitaka mahakama iendelee huku wakili wa Utetezi, Steven Kitale akisema upande huo hauoni sababu ya kuendelea na kesi hiyo na kuomba ipangiwe tarehe nyingine ili kutoa nafasi kwao kuanika sababu za kwa nini mteja wao amemtaka hakimu huyo kujiondoa katika kesi hiyo.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo, Ndyekobora ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 10,2022

Chanzo: Mwanachi
Kagame kawanyoosha hawa manabii wa kubumba Rwanda wanaigwaya kama Jehanamu. Kuna utulivuu kila mtu anakula jasho lake hakuna janjajanja ya kuuziana maji na chumvi ya upako
 
Safi sana hakim

Naona una mmudu huyo

Acha umumnyooshe mpigaji huyo

Akitoka atanyooka

Ova
 
Hakimu deal na huyu
IMG-20220727-WA0003.jpg
 
Back
Top Bottom