Hakuna aliyemfikia Molinga hadi sasa pale Yanga

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Nchimbi ametimiza mwaka hajui goli ni nini. Sarpong aliyebebwa kama mfalme na baadhi yao ana goli nne karibu msimu unaisha.

Pamoja na papaa kutopewa nafasi lakini alikuwa na jumla ya magoli zaidi ya 10. Ukichukua na magoli ya mashindano mengine alikuwa na zaidi ya magoli 15.

Laana ya papaa itawatesa sana.
 
Papaa alikuwa anapangwa dakika chache ila amefunga magoli mengiii.

Kina sarpong wanaanza kwenye timu na mara nyingi wanacheza full time ila goli hawafungi.. hata kosa kosa za hatari za kugongesha mwamba hawana.

Na yanga hii ya kisinda na carinho na mukoko molinga angepewa nafasi angefunga sana na sana
 
Utopolo wameuza AK 47 kununua upinde na mishale,hovyo kabisa wamebakia kulalamika kama changudoa aliyekopwa
 
Dah!! Ila tangu Mwinyi Zahera amuuze Makambo, na mkataba wa Tambwe uishe, Yanga imejikuta ina washambuliaji butu mpaka basi!!

Nchimbi, Sarpong, Waziri Junior, Fiston, na wengineo wengi, hakika wame prove failure! Mimi ni shabiki wa Yanga. Na katika hili nakubali, Yanga tuna washambuliaji butu na pia hatuna viungo washambuliaji wabunifu aina ya Chama, Louis,nk!!
 
Usipotumia vile vilevi vyako vya hatari unakuwaga na busara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…