Hakuna celebrities wengine Tanzania zaidi ya hawa wawili

eti hollwood haha, sikatai Kanumba alikuwa mkubwa sana ila kwa kasi ya diamond angekuwa hai alikuwa anafunikwa hata yeye, sema mtu akifa anashobokewa sana
 
Tena kwenye msiba wake watu wanasahau majonzi wanamshangaa diamond
nakumbuka hilo tukio, diamond alizua kizaazaa msiban, magazeti ya Shigongo shahidi
 
Kanumba kabla hajafa alikuwa anawafunika wote.Nadhani angekuwepo leo angekuwa namba one star in Tanzania.
Usimsingizie marehemu. R.I.P Kanumba. Kwa sasa moto wa diamond platinum ni mkubwa sana. Na ndio maana kila mtu anajitahidi kuanzisha naye beef ili aweze naye kutoka na kusikika.
 
Hata Kanumba alivyokuwa hai watu walimkejeli na kumuona si lolote, Diamond na hakika atamwagiwa sifa nyingi zaidi ya Kanumba akifa Kanumba na ray , Kanumba na lugha ya Kiingereza. Kanumba utanyonya wangapi kwenye movie??, Kanumba ze greit, Kanumba ndani ya Big Brother House 2009
 
Sipingi Diamond kupiga hatua,lakini kama kanumba angeishi miaka mitano zaidi,hakika angezua gumzo na tafrani kubwa sana.Hata huyo diamond kuna nyuzi nyingi tu za kumponda,pitia humu Jf
 
Usimsingizie marehemu. R.I.P Kanumba. Kwa sasa moto wa diamond platinum ni mkubwa sana. Na ndio maana kila mtu anajitahidi kuanzisha naye beef ili aweze naye kutoka na kusikika.
soma uelewe,wewe unazungumza sasa mimi nazungumza wakati huo anakufa alikuwa celebrity mkubwa zaidi TZ.Angeishi mpaka sasa hakika angetisha sana
 
eti hollwood haha, sikatai Kanumba alikuwa mkubwa sana ila kwa kasi ya diamond angekuwa hai alikuwa anafunikwa hata yeye, sema mtu akifa anashobokewa sana
Ndiyo,Hollywood.Kama hujui uliza,sio kuleta mipasho.Hata yeye angekuwa hai angekuwa na kasi yake.Ni nani aliyeleta mabadiliko katika industry ya filamu Tz?Jibu ni Kanumba,wakati Diamond hajapata fursa ya kushirikiana na wanamuziki wakubwa Africa kanumba alikuwa ameshashirikiana na waigizaji bora Africa kama akina Ramsey na tayari milango ilikuwa imefunguka na alikuwa anaelekea marekani kufanya movie Hollywood,ukweli ndio huo.
 
ni upepo tu kuwa mvumilivu baada ya miaka kama 5 hivi mambo haya yataisha kabisa.

Ila next time usiwafungulie Thread unazidi kuwapa kichwa wafungulie thread wakina Samatta
 
soma uelewe,wewe unazungumza sasa mimi nazungumza wakati huo anakufa alikuwa celebrity mkubwa zaidi TZ.Angeishi mpaka sasa hakika angetisha sana
Wewe ungejuaje kama Angetisha? Au ni msoma nyota wewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…