Siasa ndio ilivyo watu wanashindwa kuelewa tu unatakiwa kupinga ndio democrasia lakini lazima wanachokipinga lazima kieleweke kwa jamii mfano mimi waliompinga Mbowe kwenye uchaguzi amban sio mamluki niliwaelewa sana.
Umenena mkuu utoto na ubinafsi unawasumbua
Siasa ndio ilivyo watu wanashindwa kuelewa tu unatakiwa kupinga ndio democrasia lakini lazima wanachokipinga lazima kieleweke kwa jamii mfano mimi waliompinga Mbowe kwenye uchaguzi amban sio mamluki niliwaelewa sana.
Mtu kama sumaye naye eti unaona anataka kupinga na kujifanya mpinzani upumbavu, Mbunge chama kinakubeba watu wanaumia unashinda ubunge kwenye tundu la sindano halafu brand yako iliyokupeleka bungeni unaigeuka mimi ningewafuta Uanachama wote na kuwafukuza mala moja.
Yaani unauza utu wako unanunuliwa kizembe halafu unafikiria utasalimika kama uyo wa Tunduma ajipange sana pale Ccm ilishafutika vijana wa pale asipokuwa makini watamchinja kwa usaliti.
Ni kweli umeongea jambo la maana sana ambalo wanasiasa walio upande wa vyama vya upinzani wanatakiwa kujifunza. Hata mimi nasisitiza kuwa hakuna chama cha siasa popote pale duniani ambacho kinaweza kukubali wadau wake waende tofauti na maazimio ya chama either unayakubali au huyakubali.
Tena sijapendezwa kabisa na Silinde kwa jinsi alivyokuwa anaongea kwa kumtaja Mwenyekiti wake Mbowe kwa dharau utafikiri wanafanana umri. Sio vizuri hata kidogo. Wajifunze kwa wabunge wenzao wa CCM naamini kuna mambo mengi ya kijinga ambayo chama chao kinalazimishwa yafuatwe hali ya kuwa wanaona kabisa kuwa si sahihi, ila kwa kuheshimu maslahi ya chama wanaamua tu kukubaliana nayo wote kwa kuwa kitu kimoja.
Halafu Silinde na kampani yake hivi hawashangai kwanini wanaoshabikia wao kwenda Bungeni ni watu wa CCM and company?
Ni hayo tu.
Unayaandika haya kana kwamba hao unaowaeleza hawayajui?Watanzania hasa vijana ambao tunaingia kwenye siasa, lazima tujipange kiuchumi , kimaisha , kiakili pia. Wabunge kama silinge na Lijuakali ambao walionekana ni wabunge vijana leo njaa zinawafanya watii amri za ccm.Hatuhitaji vijana radical ila tunahitaji vijana wanao jielewa na wenye misimamo, Siasa ni kufanya kile unakiamini kupitia chama chako ambacho umechagua kuwa mwanachama.
Kwa kweli nakumbuka kauli ya kila mmoja kambale ndani ya chadema.Hivi hata chain of command hawaijui'There is a silver lining to every cloud' - timing ni nzuri kwao na kwa CHADEMA.
Kwa nini CHADEMA wawalalamikie wabunge kama hao wanaosaidia kusafisha chama!
Adui mkubwa kwa CHADEMA ni kiongozi/mwanachama mnafiki. Asiyeamini chochote kinachosimamiwa na chama, lakini anaendelea kuwemo humo kwa mategemeo ya kuvuna kesho na keshokutwa. Hana 'commitment' yoyote na chama, bali anasubiri tu kuvuna kupitia kwenye chama.
Silinde ni mfano mzuri, kwa sababu kajieleza na ameeleweka.
Pamoja na kwamba ni vigumu sana kuwatambua watu kama hawa kuwemo ndani ya chama, lakini kuna umhimu wa chama kuwa na vigezo vya msingi vya kuwapima wanachama wao, hasa kabla ya kuwapa uongozi ndani ya chama chao.
Silinde alikuwa kwenye kikao kilichofikia maamuzi hayo!Au unaishi dunia gani?Unapata wapi nguvu ya kutetea maamuzi ya mfukoni hata Kama ni Mwenyekiti wako?
Naamini katika kuimarisha na kukuza demokrasia, vikao ndio njia ya kufikia maamuzi ya pamoja. Kwa nini Mwenyekiti akisema leo tutafanya hiki au kile ,bila kuhoji mnafanya bila kuangalia athari zake. We need Patriotic democratic system
Wanashangiliwa sana na wabunge wa CCM. hawajiulizi kwa nini!Ukitaka kuwa huru Ni bora usijiunge Na chama cha siasa, vinginevyo tabu inakuhusu.Ukipingana Na viongozi au maamuzi ya chama chako, Ni usaliti.wale wabunge Wa upinzani wanadanganywa Na wanaccm eti wanajitambua.Hatari sana.Ccm ndo wasingevumilia kamwe wabunge wangeenda kinyume.binafsi nampongeza kubenea.Amejua nini maana ya mamlaka.
Jana nimemsikiliza selasini nilishangaa sana, anasema yeye bado Ni mbunge mtiifu Wa chadema huku akiponda uamuzi Wa chama chake.Kwa kweli kama Ni unafiki selasini Ni noma.Hivi hats chain of command anaijua kweli.Wanashangiliwa sana na wabunge wa CCM. hawajiulizi kwa nini!
Magu mwenyewe aliwahi kusema ukiona mpinzani wako anakusifia sana jiulize mara mbili, kuna mahali utakuwa unakosea.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kiukweli nahisi tangu nimejiunga JF sijawahi kukutana na hoja yenye facts za ukweli wa hali halisi kama hiiWABUNGE VIJANA JIFUNZENI KUWA WATII KWA VYAMA VYENU, HAKUNA CHAMA DUNIANI AMBACHO KINA ENDEKEZA YEYOTE AMBAYE HATII MAAZIMIO YA CHAMA HATA KAMA HAKUBALIANI NAYO. CCM NI MFANO MZURI. MUDA HUU WOTE WAPO BUNGENI KWA SABABU MWENYEKITI AU CHAMA KIMEWATAKA WAENDELEE KUWA BUNGENI PAMOJA NA KWAMBA KUNA WENGI HATA USINGIZI HAWALALI KWA HOFU YA KUFA NA CORONA.
Wabunge wanao jiunga na vyama vya upinzania waache njaa, Hakuna chama duniani ambacho huwa kinamwacha yeyote ambaye anakwenda kinyume na matakwa ya chama, Iwe Marekani, Russia, China au mashariki ya kati , mambo ni yale yale lazima kutii jambo lilo kubalika na chama chako.
Hawa Vijana ambao wanakiuka makubaliano ya vyama vyao na kushangiliwa na Chama Cha Mapinduzi, wnadhani mle CCM hakuna wabunge ambao huwa hawaikubali kauli ya mwenyekiti, wakati uhalisia chama cha mapinduzi ndio chama ambacho huwezi pingana na maamuzi ya chama au ya mwenyekiti.
Katika sakata hili la juzi, inaonyesha wale wabunge kina Silinde, Lijuakali, etc ambao wamaamua mkulinda posho zao kwa kisingizio wananchi ndio waliowachagua ni kiishiwa kisiasa na kukosa mwelekeo, hakuna chama wataaenda kitaendekeza ujinga kama huu.
Kuwa mwanachama ni Pamoja na kutetea maslahi ya chama hata kama hukubaliano nao.
Watanzania hasa vijana ambao tunaingia kwenye siasa, lazima tujipange kiuchumi , kimaisha , kiakili pia. Wabunge kama silinge na Lijuakali ambao walionekana ni wabunge vijana leo njaa zinawafanya watii amri za ccm.Hatuhitaji vijana radical ila tunahitaji vijana wanao jielewa na wenye misimamo, Siasa ni kufanya kile unakiamini kupitia chama chako ambacho umechagua kuwa mwanachama.
- Unadhani wana ccm wanamkubali Magufuli kwa kila anancho waambia waseme au wafanye, ila kwa sababu wamekubali kuwa wanachama basi sharti lake lazima kuheshimu kauli ya kiti cha mwenyeketi au ya chama.
- Silinge na wenzie wanadhani Republic kule marekani wanamkubali sana trump hata kuendelea na vikao wakati democrat wamsusia vikao?
- Silinde na wenzake wanadhani wabunge wa ccm hawaogopi corona wakati kuna Ushahidi kuna wabunge wamepoteza maisha? No, Ila kwa sababu mwenyekiti anawahitaji wakae bungeni.
- CCM umefukuza wanachama wengi sana kwa kutotii kauli ya chama au ya mwenyekiti hata wengine hawajulikani walipo.
- Huwezi kuwa mwana siasa kama huwezi kusimamia maazimio ya chama .
Sitegemee silinde na lijuakali kurudi bungeni, wakibebwa na CCM wajue hawata kuwa na uhuru Zaidi ya kuunga hoja za serikali hata wakati wa mambo ya hovyo.
Msimamo ni kipimo cha utu.
Tabutupu
CEO, Tabutupu Group
Paris, France| Nyaishoshi Tanzania