Hakuna chama duniani kinaendekeza wasiotii maazimio ya chama/ Mwenyekiti wake

Hakuna chama duniani kinaendekeza wasiotii maazimio ya chama/ Mwenyekiti wake

Tumewachoka na masimango yenu kwa vijana, vijana hamuhitajiki humo endeni nje. Wabaki wenyewe sifiasifia Mbowe. By the way kaeni ndani muyaongee wenyewe na sio kila MTU anaibuka na statement yake hiyo sio nidhamu na ni double standard
Haahaa vijana sijui wakimbilie wapi, mavyama yote yako hivi lazima ulambe viatu vya wakubwa sio ccm wala upinzani.Bora kungekuwa Na mgombea huru.
 
Kiukweli nahisi tangu nimejiunga JF sijawahi kukutana na hoja yenye facts za ukweli wa hali halisi kama hii

Umeongea hali halisi na ukweli wa nafsi jinsi ulivyo na sio sanaa za maigizo wanazotuletea hao wabunge walio mkaidi Mbowe

Mwenye akili finyu ataona nakudhani wao ni kweli wanapigania wananchi uwakilishi wawananchi wao bali ni njaa, usaliti na unafiki



Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo watu wanataka uongozi bila kujua ethics za uongozi.Kuna kitu kinaitwa principles of leadership and management, mojawapo Ni Chain of command. Vijana wajifunze kwanza
 
Silinde alikuwa kwenye kikao kilichofikia maamuzi hayo!Au unaishi dunia gani?
Nimekuta naikumbuka ghafla ile kama aliyokuwepo Lema,akiwa gerezani walienda kumtembelea kinyume na maelekezo ya mwenyekiti Magufuli ambaye aliwaona kama wasaliti!

Baada ya tukio hilo kamari nzima ililazimishwa kujiuzulu na kupewa onyo kali kwa kwenda kumtembelea mwana kamati mwenzao gerezani!

Sasa mbunge wa CCM ajaribu kuamua kutohudhuria bunge kisa Corona,nadhani anavuliwa uanachama wake siku hiyo hiyo!
Watu wamesahau wabunge Wa ccm walipigwa marufuku kwenda kumtembelea lissu Nairobi, Na watu walitii agizo.Kilichofanywa Na kina silinde sio cha kuigwa Na vijana.Ni usaliti.
 
Unapata wapi nguvu ya kutetea maamuzi ya mfukoni hata Kama ni Mwenyekiti wako?

Naamini katika kuimarisha na kukuza demokrasia, vikao ndio njia ya kufikia maamuzi ya pamoja. Kwa nini Mwenyekiti akisema leo tutafanya hiki au kile ,bila kuhoji mnafanya bila kuangalia athari zake. We need Patriotic democratic system
Hivi anacho sema mwenyekiti wa ccm huwa mnapinga?? Acha unafiki

Sent by IPhone
 
Ukitaka kuwa huru Ni bora usijiunge Na chama cha siasa, vinginevyo tabu inakuhusu.Ukipingana Na viongozi au maamuzi ya chama chako, Ni usaliti.wale wabunge Wa upinzani wanadanganywa Na wanaccm eti wanajitambua.Hatari sana.Ccm ndo wasingevumilia kamwe wabunge wangeenda kinyume.binafsi nampongeza kubenea.Amejua nini maana ya mamlaka.
Mkuu hakuna anae wadanganya wao wanajua wakitakacho. CDM iwaangalie kwa ukaribu. Wengi wao walisha tajwa humu na wengine kati yao wako kwenye list ya Mbatia au walishatangaza kukihama chama. Sioni tatizo ni nini ukiacha wale wanaokwenda mbali zaidi na kukipigia kelele chama na mwenyekiti wao. Hao kuna vyombo vya nidhamu ndani ya chama.
CCM wamepata propaganda hata kundu lao hawalioni .
Mwisho ya yote vyama vyote vinatawaliwa na " iron rule of oligarchy" na pia demokrasia ina hitaji ushirikishi kuendana na katiba husika.
 
WABUNGE VIJANA JIFUNZENI KUWA WATII KWA VYAMA VYENU, HAKUNA CHAMA DUNIANI AMBACHO KINA ENDEKEZA YEYOTE AMBAYE HATII MAAZIMIO YA CHAMA HATA KAMA HAKUBALIANI NAYO. CCM NI MFANO MZURI. MUDA HUU WOTE WAPO BUNGENI KWA SABABU MWENYEKITI AU CHAMA KIMEWATAKA WAENDELEE KUWA BUNGENI PAMOJA NA KWAMBA KUNA WENGI HATA USINGIZI HAWALALI KWA HOFU YA KUFA NA CORONA.

Wabunge wanao jiunga na vyama vya upinzania waache njaa, Hakuna chama duniani ambacho huwa kinamwacha yeyote ambaye anakwenda kinyume na matakwa ya chama, Iwe Marekani, Russia, China au mashariki ya kati , mambo ni yale yale lazima kutii jambo lilo kubalika na chama chako.

Hawa Vijana ambao wanakiuka makubaliano ya vyama vyao na kushangiliwa na Chama Cha Mapinduzi, wnadhani mle CCM hakuna wabunge ambao huwa hawaikubali kauli ya mwenyekiti, wakati uhalisia chama cha mapinduzi ndio chama ambacho huwezi pingana na maamuzi ya chama au ya mwenyekiti.

Katika sakata hili la juzi, inaonyesha wale wabunge kina Silinde, Lijuakali, etc ambao wamaamua mkulinda posho zao kwa kisingizio wananchi ndio waliowachagua ni kiishiwa kisiasa na kukosa mwelekeo, hakuna chama wataaenda kitaendekeza ujinga kama huu.

Kuwa mwanachama ni Pamoja na kutetea maslahi ya chama hata kama hukubaliano nao.

  • Unadhani wana ccm wanamkubali Magufuli kwa kila anancho waambia waseme au wafanye, ila kwa sababu wamekubali kuwa wanachama basi sharti lake lazima kuheshimu kauli ya kiti cha mwenyeketi au ya chama.
  • Silinge na wenzie wanadhani Republic kule marekani wanamkubali sana trump hata kuendelea na vikao wakati democrat wamsusia vikao?
  • Silinde na wenzake wanadhani wabunge wa ccm hawaogopi corona wakati kuna Ushahidi kuna wabunge wamepoteza maisha? No, Ila kwa sababu mwenyekiti anawahitaji wakae bungeni.
  • CCM umefukuza wanachama wengi sana kwa kutotii kauli ya chama au ya mwenyekiti hata wengine hawajulikani walipo.
  • Huwezi kuwa mwana siasa kama huwezi kusimamia maazimio ya chama .
Watanzania hasa vijana ambao tunaingia kwenye siasa, lazima tujipange kiuchumi , kimaisha , kiakili pia. Wabunge kama silinge na Lijuakali ambao walionekana ni wabunge vijana leo njaa zinawafanya watii amri za ccm.Hatuhitaji vijana radical ila tunahitaji vijana wanao jielewa na wenye misimamo, Siasa ni kufanya kile unakiamini kupitia chama chako ambacho umechagua kuwa mwanachama.

Sitegemee silinde na lijuakali kurudi bungeni, wakibebwa na CCM wajue hawata kuwa na uhuru Zaidi ya kuunga hoja za serikali hata wakati wa mambo ya hovyo.

Msimamo ni kipimo cha utu.

Tabutupu
CEO, Tabutupu Group
Paris, France| Nyaishoshi Tanzania

Ukiwa baba mkorofi unawashirikisha watoto kila siku mnatukana majirani, unawafundisha ukosefu wa nidhamu dharau na mengineyo mabaya, ipo siku watakurudia wewe mwenyewe, utukanwe udharauliwe hata kichapo pia maana hayo ndio uliyowafundisha. Sasa chama kiyavumilie tu maana mafundisho mliwapa wenyewe.
 
Ni kweli umeongea jambo la maana sana ambalo wanasiasa walio upande wa vyama vya upinzani wanatakiwa kujifunza. Hata mimi nasisitiza kuwa hakuna chama cha siasa popote pale duniani ambacho kinaweza kukubali wadau wake waende tofauti na maazimio ya chama either unayakubali au huyakubali.
Tena sijapendezwa kabisa na Silinde kwa jinsi alivyokuwa anaongea kwa kumtaja Mwenyekiti wake Mbowe kwa dharau utafikiri wanafanana umri. Sio vizuri hata kidogo. Wajifunze kwa wabunge wenzao wa CCM naamini kuna mambo mengi ya kijinga ambayo chama chao kinalazimishwa yafuatwe hali ya kuwa wanaona kabisa kuwa si sahihi, ila kwa kuheshimu maslahi ya chama wanaamua tu kukubaliana nayo wote kwa kuwa kitu kimoja.
Halafu Silinde na kampani yake hivi hawashangai kwanini wanaoshabikia wao kwenda Bungeni ni watu wa CCM and company?
Ni hayo tu.
Hatuwaombei mabaya lkn yasijeyakawakuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa baba mkorofi unawashirikisha watoto kila siku mnatukana majirani, unawafundisha ukosefu wa nidhamu dharau na mengineyo mabaya, ipo siku watakurudia wewe mwenyewe, utukanwe udharauliwe hata kichapo pia maana hayo ndio uliyowafundisha. Sasa chama kiyavumilie tu maana mafundisho mliwapa wenyewe.
Kwa hoja yako hats Jpm inamuhusu mwenyekiti Wa ccm
 
Tafuta chama ambacho kina demokrasia kama unayonisema.. hata chama cha trump huwezi fanyabujinga wa kina silinde
Unapata wapi nguvu ya kutetea maamuzi ya mfukoni hata Kama ni Mwenyekiti wako?

Naamini katika kuimarisha na kukuza demokrasia, vikao ndio njia ya kufikia maamuzi ya pamoja. Kwa nini Mwenyekiti akisema leo tutafanya hiki au kile ,bila kuhoji mnafanya bila kuangalia athari zake. We need Patriotic democratic system

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Selasini kafika mwisho.. aende akamwulize kafulila.. ikisha anza kuwa malaya, lazima upoteze utuu wako.

Msimamo ni kipimo cha utu.
Jana nimemsikiliza selasini nilishangaa sana, anasema yeye bado Ni mbunge mtiifu Wa chadema huku akiponda uamuzi Wa chama chake.Kwa kweli kama Ni unafiki selasini Ni noma.Hivi hats chain of command anaijua kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hoja yako hats Jpm inamuhusu mwenyekiti Wa ccm

Basi tulieni muachieni mwenyekiti apambane na zigo lake, watu wamechoka kufundishwa ujinga, wanataka tafasiri halisi ya Chama Cha Demokrasia na Maendelo kwa vitendo.
 
Tusiwalaumu waliohudhuria bungeni,binafsi nimewaelewa;
1.) Hawajashiriki vizuri migogoro ya chadema na serikali hata wenzao walipokuwa lock-up hawakwenda.
2.) Wanajua chama hakitowapitisha kugombea
*(3.) Wanafahamu hata wakigombea hawafui dafu kwa wagombea wa Ccm (hawarudi tena bungeni).
4.) Walikuwa wanamheshimu sana selasini na mbowe walimwona mbabe sasa wanamwoneshea mwishoni.
**(5.)wanaogopa kupoteza posho lakini zaidi kiinua mgongo kinaweza kukatwa kibabe na wasiwe na chakifanya hats mahakamani.
6.)wanatafuta utiifu ili wapokewe na vyama vingine kama Ccm ama Nccr.
Kwenye siasa unapaswa kujua kuwa kigeugeu,kutoona aibu,kuongelea yeyote mbovu hata babaako,kujipendekeza nk
 
Mkuu @Kalamu1,kongole sana kwa mchango wako bora sana. Hapa umeandika kila kitu cha msingi,na hakika umemaliza.
Ubarikiwe.
'There is a silver lining to every cloud' - timing ni nzuri kwao na kwa CHADEMA.

Kwa nini CHADEMA wawalalamikie wabunge kama hao wanaosaidia kusafisha chama!

Adui mkubwa kwa CHADEMA ni kiongozi/mwanachama mnafiki. Asiyeamini chochote kinachosimamiwa na chama, lakini anaendelea kuwemo humo kwa mategemeo ya kuvuna kesho na keshokutwa. Hana 'commitment' yoyote na chama, bali anasubiri tu kuvuna kupitia kwenye chama.
Silinde ni mfano mzuri, kwa sababu kajieleza na ameeleweka.

Pamoja na kwamba ni vigumu sana kuwatambua watu kama hawa kuwemo ndani ya chama, lakini kuna umhimu wa chama kuwa na vigezo vya msingi vya kuwapima wanachama wao, hasa kabla ya kuwapa uongozi ndani ya chama chao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni kwamba John ana miaka kama 5 tuu aondoke.. lakini maisha ya siasa ni zaidi ya miaka 5.

Wanao kupa ridhaa ni wananchi, lakini hawa wananchi ni wananchama wa chama husika.

Ukizingua chama upo hatarini kuzinguliwa na wananchama pia.
Tusiwalaumu waliohudhuria bungeni,binafsi nimewaelewa;
1.) Hawajashiriki vizuri migogoro ya chadema na serikali hata wenzao walipokuwa lock-up hawakwenda.
2.) Wanajua chama hakitowapitisha kugombea
*(3.) Wanafahamu hata wakigombea hawafui dafu kwa wagombea wa Ccm (hawarudi tena bungeni).
4.) Walikuwa wanamheshimu sana selasini na mbowe walimwona mbabe sasa wanamwoneshea mwishoni.
**(5.)wanaogopa kupoteza posho lakini zaidi kiinua mgongo kinaweza kukatwa kibabe na wasiwe na chakifanya hats mahakamani.
6.)wanatafuta utiifu ili wapokewe na vyama vingine kama Ccm ama Nccr.
Kwenye siasa unapaswa kujua kuwa kigeugeu,kutoona aibu,kuongelea yeyote mbovu hata babaako,kujipendekeza nk
20200506_002342.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana wale hawawezi kazi kumbuka katika siasa unatakiwa usimame upande wako..wale wameshikwa na tamaa na uwoga bora wafutwe uanachama na tamaa zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom