Hakuna chama kilichotamba duniani kama Baath Party

Hakuna chama kilichotamba duniani kama Baath Party

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Kwenye kilele cha kutamba kwao ushindi wa asilimia 98 ilikuwa kawaida sana.

Ilikuwa Sherehe nchi nzima wakishatangazwa washindi.

Ungeweza fikiria ni kweli wanaungwa mkono Kwa asilimia 99.

Chama cha Baath nchini Iraq kilikuwa kimeshika hatamu kweli kweli.

Leo ni historia tu baada ya kufutwa na kupigwa marufuku.

Iraq haijapata tena ona chama kinachoshinda Kwa asilimia 99.

Sasa demokrasia imeshamiri na vyama mbali mbali vinatoa wabunge.

Na Serikali inaundwa wakati mwingine Kwa vyama mbalimbali kushirikiana.

Siku moja na huku yatafika
 
Nazi. Sijui kama nimetaja vizuri. Hao jamaa waliua vibaya sana.

Kiufupi.

HAKUNA JAMBO JIPYA DUNIANI.

"Wasiosoma ni chakula cha wasomi, wasomi Ni chakula cha wanasiasa, wanasiasa Ni chakula cha wafanyabiashara".
 
Bila ya Wamarekani kuivamia Iraq na kuipindua serikali ya Saddam Hussein, yawezekana chama cha Ba’ath huenda bado kingekuwa madarakani mpaka leo hii.

Kwa Tanzania, labda nasi tuvamiwe na Wamarekani halafu waitoe CCM madarakani na baadaye ipigwe marufuku kabisa.

Lakini hatujafika huko bado. Na mazingira ni tofauti sana.

Hata ujasiri wa kuwa na Orange Revolution kama ile ya Ukraine mwaka 2004 - 2005 au ile Arab Spring, hatuna.

Wa Ukraine waliingia barabarani baada ya uchaguzi wa run-off kutokuwa wa huru na haki.

Waliandamana kwa miezi miwili bila kuchoka mpaka kikaeleweka.

Sisi ujasiri wetu upo kwenye mitandao tu.
 
Hatujafika huko bado. Na mazingira ni tofauti sana.

Hata ujasiri wa kuwa na Orange Revolution kama ile ya Ukraine mwaka 2004 - 2005 au ile Arab Spring, hatuna.

Wa Ukraine waliingia barabarani baada ya uchaguzi wa run-off kutokuwa wa huru na haki.

Waliandamana kwa miezi miwili bila kuchoka mpaka kikaeleweka.

Sisi ujasiri wetu upo kwenye mitandao tu.

Ingawa wewe ni CCM lakini kwa hili umesema ukweli mtupu.
 
Nazi. Sijui kama nimetaja vizuri. Hao jamaa waliua vibaya sana.

Kiufupi.

HAKUNA JAMBO JIPYA DUNIANI.

"Wasiosoma ni chakula cha wasomi, wasomi Ni chakula cha wanasiasa, wanasiasa Ni chakula cha wafanyabiashara".
Wasiosoma Ni Chakula cha Wasomi, Wasomi ni Chakula cha Wanasiasa, Wanasiasa ni Chakula cha Waganga wa Jadi(Washirikina)
 
Mimi siyo CCM. Kamwe sijawahi kuwa CCM.
Si kila anayewakosoa CHADEMA na wapinzani wengine, ni CCM.
Btw, hata CCM huwa nawakosoa sana tu.
Unabisha?
Hapa Mkuu umesema kweli kabisa, ww ni Mtanzania mwenye uchungu na Nchi yako

Humo humo ndani ya CCM watatoka wapinzani na wala si muda mrefu.

Humu tuliopo nyuma ya mitandao tuna kelele sana

Wakati Uchaguzi na kufikia ushindi ni KUHESABU KURA sio kupiga na kuwahi mitandao
 
Siwezi kuisifia demokrasia ya Iraq hii ambayo Iran ana influence na makundi ya kijeshi upande wake uku akitaka baadhi ya mawaziri watoke block yake. US naye ana influence na anataka wamfuate yeye. Kisha baadae Iraq ndio inaambulia makombo ya kuamua mustakabari wao.

Tazama PM wao mpya anavyohangaika kubalance influence. PM aliyeondoka alipigwa vita kwa vile ana mafungamano na Iran. Rais alimkataa Waziri Mkuu juzijuzi hapa.

Siasa zao hazina tofauti sana na za Lebanon.
 
Uelewa wa Watanzania (baadhi) kuhusu Siasa za Kidunia ni mdogo sana, sasa unawezaje kulinganisha Baath na CCM kwa mfano? USA alivamia Irak kumuondoa Sadamu Husseni na siyo kukiondoa Chama cha Baath, sasa USA avamie Tanzania kumuondoa nani? na Kwa sababu gani? Magufuli anamaliza muda wake 2025, sasa USA ivamie kuondoa CCM?

CCM ni ni kwanza? CCM ni Taasisi na siyo mtu, na mnafikiri ni uamuzi rahisi kwa USA kutumia Majeshi yake kuivamia nchi nyingine ambayo siyo threat kwa namna yoyote ile kwa USA? Ni Raisi gani wa USA atakuwa mjinga hivyo?

Jielimisheni kwanza Siasa za Kidunia zinavyokwenda kama ingekuwa rahisi kivivyo si wangeshavamia Uganda kwanza kumuondoa Museveni au unafikiri ni ninyi tu ndiyo wenye malalamiko hapa Duniani?
 
Uelewa wa Watanzania (baadhi) kuhusu Siasa za Kidunia ni mdogo sana, sasa unawezaje kulinganisha Baath na CCM kwa mfano? USA alivamia Irak kumuondoa Sadamu Husseni na siyo kukiondoa Chama cha Baath, sasa USA avamie Tanzania kumuondoa nani? na Kwa sababu gani? Magufuli anamaliza muda wake 2025, sasa USA ivamie kuondoa CCM? CCM ni ni kwanza? CCM ni Taasisi na siyo mtu, na mnafikiri ni uamuzi rahisi kwa USA kutumia Majeshi yake kuivamia nchi nyingine ambayo siyo threat kwa namna yoyote ile kwa USA? Ni Raisi gani wa USA atakuwa mjinga hivyo?

Jielimisheni kwanza Siasa za Kidunia zinavyokwenda kama ingekuwa rahisi kivivyo si wangeshavamia Uganda kwanza kumuondoa Museveni au unafikiri ni ninyi tu ndiyo wenye malalamiko hapa Duniani?
💯%.
 
Wewe ndo Una unaelewa mdogo kabisa
Wapi nimesema CCM Sawa na Baath?
Au wapi nilisema naomba USA wavamie kuitoa CCM?
Jitulize ..usivamie kila unachokiona
 
Bila ya Wamarekani kuivamia Iraq na kuipindua serikali ya Saddam Hussein, yawezekana chama cha Ba’ath huenda bado kingekuwa madarakani mpaka leo hii.

Kwa Tanzania, labda nasi tuvamiwe na Wamarekani halafu waitoe CCM madarakani na baadaye ipigwe marufuku kabisa.

Lakini hatujafika huko bado. Na mazingira ni tofauti sana.

Hata ujasiri wa kuwa na Orange Revolution kama ile ya Ukraine mwaka 2004 - 2005 au ile Arab Spring, hatuna.

Wa Ukraine waliingia barabarani baada ya uchaguzi wa run-off kutokuwa wa huru na haki.

Waliandamana kwa miezi miwili bila kuchoka mpaka kikaeleweka.

Sisi ujasiri wetu upo kwenye mitandao tu.

Ukisoma vizuri my point sio kuwa tungojee USA waje waitoe CCM
My point ni kuwa during its dark days..
Hakuna aliehisi kuna siku wataondoka
Iwe by protests au by force kutoka nje
That's my point..
 
Bro ona aibu ata kidogo Iraq hii hii iliyogeuka magofu na vita ya wenyewekwa wenyewe, unaisifu ina demokrasia na inachagua wabunge wanaotakiwa.

Wewe sio Muiraq
Wao ndo wanajua kipi nafuu..
Maisha chini ya Baath na Saddam
Au sasa..unao tafiti unaosema wanajuta?
Unaweza onesha?
 
Chama cha Baathi kilikuwa mpaka Syria hawa naweza kusema ni kama taasisi walikuwa walikuwa wako katika kila idara ya serikali ni kama mfumo wa CCM sasa hivi, na ndio sababu kubwa USA walipomuondoa madarakani Saddam kosa kubwa walilolifanya ni kuvunja chama na kuwaondoa viongozi,

wanachama na wafuasi wa chama cha Baathi mpaka katika vyombo vya usalama hii ndio ikaleta balaa la muda mrefu kukawa na visasi na kama kuanza kuunda kila kitu upya maana chama kilikuwa na mizizi kila sehemu ikawa utafukuza mpaka wapi, na chama cha Baathi cha Iraq na Syria (bado kipo) hawa walikuwa sio mchezo wana majasusi kila kona ni mfumo wa maisha ya watu hujajiunga na Baathi huna nafasi kupata kazi.

Ziko clip za Saddam katika mikutano ya chama alikuwa kapata taarifa kuna viongozi walikuwa wanataka kupinga uongozi wa chama, aliwataja mbele ya watu basi ukitajwa unainuka, ukisimama tu unatolewa nje ndio unapotezwa moja kwa moja uasi ndani ya chama kama ndoto maana kuna ujasusi wa hali ya juu. Kurudi hapa kwetu ndio kama CCM,

Sote tunajuwa wafuasi wa CCM sio hawa wanaoshika kanga na kofia tu, wako kila sehemu maofisini, idara zote, vyombo vya usalama mpaka majeshi yote huwezi kupewa kitengo kama wewe sio CCM toka zamani ndio maana unaona wakistaafu kama ma judge au wanajeshi wanapewa nafasi katika serikali hata na wengine wanarudi wanakuwa majasusi ndani ya chama, hata watu wa kitengo wakistaafu wanakuja kufanya kazi za kijasusi ndani ya chama.

Kuiondoa CCM unaondoa mfumo wote wako kila sehemu na wao wanajuwa hilo ndio maana hawatumii nguvu sana katika kampeni. usisikie hizi story za viongozi wa usalama kuwa hatuna chama tunasimamia amani tu hilo hakuna wote viongozi wote wa vyombo vya usalama na maofisi yote idara zote wako na wanafanya kazi kuhakikisha kila kitu under control.

Kwa ufupi kuiondoa CCM ni kama kuiondoa Baathi na kuna gharama. KANU kenya waliondolewa sababu hawakuwa na mfumo kama wa CCM na zaidi KANU iliondolewa na wana KANU wenyewe wamejigawa tu nje lakini ni walewale kina Kenyata, Mudavadi na wengine wengi hakuna jipya ni kama kwenda mahakamani kubadili jina lako kisheria lakini utabaki yuleyule.
 
Back
Top Bottom