Hakuna chuki mbaya kama ya ndugu wa damu. Je, wewe imewahi kukutokea na ulitatuaje hili tatizo?

Hakuna chuki mbaya kama ya ndugu wa damu. Je, wewe imewahi kukutokea na ulitatuaje hili tatizo?

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
kumekuwa na Kesi nyingi za kaka na dada, mama na mtoto, baba na mama yani ni hatari.

Inafikia Hatua hadi wanatamkiana maneno mabaya.

Kesi nyingi Mahakamani ni za ndugu aidha wakigombea mirathi, Ardhi au mambo mengine.

Tumalize Chuki na tujenge Umoja ili shetani asipate nafasi.
 
Mifarakano Mara nyingi hutokea katika familia masikini.
Kwa matajiri Kuna upendo na umoja na ikitokea wametofautiana huwa wanaitisha kikao na kusuluhisha mara moja.

Ila Kwenye familia masikini Ni chuki,wivu na majungu mwanzo mwisho.

My Take: Jamani tupambane Sana tupigane na umasikini kwa sababu ndio chanzo kikuu cha mifarakano katika familia nyingi.
 
Umaskini ni mavi...ni laana kubwa sana...
Huwez kukuta upumbav huo kwa matajiri..kwanza kila.mtu yuko bize, madili mengi ya pesa, huo muda mchafu wa kugombana sjui unapatikana wapi, sanasana wanakutana kusherekea mafanikio ya utajiri wao
 
Ilitokea mimi kwa Mdogo wangu anayenifuata, Dah tulisuluhisha ila nilichojifunza ni kuishi naye kwa akili kubwa sana

Pili ilitokea kwa sister mtoto wa baba mkubwa, Dah mpaka leo makaa na ndugu mbali sana, nitamsaidia mtu akiwa kwake na sio ukaribu...hili limefanya tunaheshimiana mpaka leo
 
kuna nadharia wabongo tumekariri sana kwamba ndugu ni maadui

watu wengi wana mabaya ya kusimulia kuhusu ndugu

ila ukifuatilia unakuta ni upuuzi mtupu mambo ya kutopigiana simu ama kutotumiana hela ama kuna hii ya kawaida sana; kisa ndugu flani hakumaliza shule/hakuoa/hana kazi/ni mlevi basi mnaungana kumchukia....

ukimchukia mtu, mchukie kwa sababu za kueleweka basi....
 
Back
Top Bottom