jamani huo ni msiba kwangu mimi niko NSSF sasa nikiamua kuhamia ALPF ambakowana utaratibu ukijitoa wanakulipa itakuwaje, watakubali?
naomba kujua utaratibu ili nihame fasta, kwa jinsi tunavyokufa kizembe kama kibarlow, kimwangosi, kimbagala na gongolamboto kwa mabamu, meli za spice sagth zilivyozama ... hiyo miaka sitini atafikisha nani kwa mazingira hayo??
nimekuwa nikifuatilia mikutano tofauti ya tume za uchunguzi (commission of inquiry) za Kenya na moja ya vitu vinavyonivutia ni kuwa mara nyingine wanatumia vyumba vyenye kuta zilizowekwa vioo. Hii inasaidia kuwa mtu anavyokuwa anaeleza kitu anaweza kujiona kwenye kioo (yaani kama salon). Hii system inasaidia sana kumjua mtu anaposema uongo maana naye anajiona kuwa amedanganya!
Nimemuona pia Dau akiongea jana japo haihitaji utaalamu mwingi wa kujua wasema uongo huonekana vipi lakini alikuwa anasema tu kikubwa akijua kuwa pale alipo msingi wake sio haki na ukweli.
Sasa kama anataka kutwambia kuwa huu mfumo haupo kwingine ni kwa nini tusichukue pesa zetu sasa kutokana na mkataba wa zamani then wanaotaka waombe upya ambazo pesa zao zitakaa mpaka huko wanakokusema!
Inasikitisha kuwa taifa la waongo na wasiojali.
Hivi lazima kila kitu tufanane na nchi nyingine za dunia?! Hatuwezi kubuni vya kwetu kwa ajili ya maslahi yetu? Majitu mengine bwana?!
Ajira zenyewe ziko wapi? Tatizo lingine ni kuwa Mifuko yetu ya Hifadhi ya Jamii haizingatii thamani ya pesa, umechangi laki moja tangu 1960s ukistaafu wanakupatia riba ya elfu 8!Kitakusaidia nini? wakati bado una nguvu zako na unaweza kufanya kazi. Kumbuka hizo fedha zinawekwa pale utapokuwa umeishiwa na nguvu na madhara ya kupewa mapema yameonekana ndio maana kwa upande wangu naona ni bora inavyofanywa sasa kwani ukiwa hauna nguvu huna haja ya kuwa Matonya.