Hamna kitu kibaya kujiona wewe ni bora kuliko binadamu wengine na mawazo mazuri zaidi ya binadamu wengine wote waliowahi kuishi katika ulimwengu huu. Kauli ya huyu Mkurugenzi inadhihirisha kuwa yeye ni bora zaidi na mawazo yake ni bora zaidi ya wengine. Issue inayohusu maslahi ya watu (individuals) lazima iamuliwa na watu (individuals) kwa umoja wao na ndo maana issue kama ya katiba ya Jamhuri tumeruhusiwa kila mtu kutoa maoni yake mbali na kwamba wapo wanasheria waliobobea kwenye mambo ya katiba na sheria lakini hawajaachiwa wao watutungie katiba. Na katika suara zima la Fao la kujitoa ni juu ya wahusika (contributors/members) wa mifuko kuamua namna inavyofaa kuchukua fao lao pindi wanapokuwa hawana kazi. Kauli kama ya Ramadhan ni kauli ya kipuuzi ya kuingilia uhuru wa mtu binafsi kwa maslahi ya kikundi kidogo katika jamii, jambo hili halikubaliki!
Haingii akilini mtu mwenye PHD akasema eti ukiacha/kuachishwa/mkataba kuisha utafute kazi sehemu nyingine uendelee kuchangia. Huyu mtu nadiriki kusema si mtanzania na kama ni mtanzania basi hayajui maisha ya watanzania na atakuwa msaliti mkubwa katika taifa hili tajiri la watu masikini, simuhukumu kwa lolote kwa kuwa nami si wa haki aliye na haki atamhukumu. Ramadhan hata kama utafumba macho na kuziba masikio bado nafsi yako inakuhukumu kwa maneno ya kejeli na ya dharau kwa watu wasio na hatia. Nani asiyejua kuwa pesa za mifuko ya jamii serikali/ mifuko yenyewe mmeziwekeza kwenye miradi ya muda mrefu kiasi kwamba inaelekea kufilisika na hiki ndicho chanzo cha kutunga sheria ya fao la kutojitoa ambayo nayo imepitishwa bila kujadiliwa bungeni kwenye schedule of amendements? Nani asiyejua ukweli huu? Leo hii unakurupuka eti duniani kote hakuna fao la kujitoa? I doubt you might be mentally insane or forced by your lower eagle!
Ramadhan na wote wenye mitazamo sawa na Ramadhani mkumbuke vyeo mlivyonavyo ni dhamana ya muda tu ambapo sisi ndio tunawalipa mishara, ipo siku we will bring you down on our floor na ndipo nanyi mtapata kujua kuwa ubinadamu ni zaidi ya cheo na mali zisizokuwa za haki. Tutapigania haki zetu si kwa upanga au mabavu, vitisho na sheria kandamizi kama mnavyofanya bali kwa kumtumainia yule aliye wa haki naye atatupigania. Hakika Ramadhani na watu wenye mtazamo kama wako kizazi chenu hakitapita bila kushuudia adhabu ya unyanyasaji na dhuluma mlizowatendea watanzania katika taifa lao!