Columbus
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 2,002
- 651
Kitakusaidia nini? wakati bado una nguvu zako na unaweza kufanya kazi. Kumbuka hizo fedha zinawekwa pale utapokuwa umeishiwa na nguvu na madhara ya kupewa mapema yameonekana ndio maana kwa upande wangu naona ni bora inavyofanywa sasa kwani ukiwa hauna nguvu huna haja ya kuwa Matonya.
Nakushangaa!!!!!!. Hivi ni watanzania wangapi walioajiriwa kama sio idadi ndogo sana? je hao ambao hawajawahi wala hawajaajiriwa hawahitaji kuangaliwa maisha yao uzeeni? kuna utaratibu mwingine walioandaliwa watu hao?
Kuna mahitaji ya msingi kabisa ambayo hivi sasa serikali imeshindwa kutoa kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na maji safi, huduma bora za afya, usalama wa raia, elimu bora pamoja na usafiri nk nk, itakuwaje serikali hiyo hiyo iniandalie maisha bora ya uzeeni? huu ni wizi wa mchana kweupee!!
"Mtu mwenye akili akikueleza kitu cha kijinga huku akijua una akili anakudharau" mwl. J.K. Nyerere.