Hakuna Fao la Kujitoa NSSF duniani kote - Ramadhan Dau

Hakuna Fao la Kujitoa NSSF duniani kote - Ramadhan Dau

Wenyewe wanataka kutukopesha majumba. Sisi tunataka kwenda shule, tunataka kuanzisha biashara. Hatutaki riba kwenye fedha yetu. Tunataka pesa bila riba. Haiwezekani nikakupa fedha yangu halafu nikulipe riba. Kwa maana najua hakuna mkopo wa nyumb usio na riba. Mimi ninataka fedha yangu kama ilivyo. Nikifilisika ni mimi. Wao ni nani hata wanionee huruma? Mbona watu wanaiba kwenye gesi na hawatuonei huruma? Fedha zetu zina nini? Watuonee huruma kwenye hili tu. Hebu waache kutuchezea akili zetu. Tunataka fedha zetu!
 
Wangeiga china kupiga risasi mafisadi hadharani hili la fao uzeeni kufikisha miaka 55 ningelikubali. Ukweli ni kuwa nssf ipo taabani financially kutokana ni keherehere chao cha kuwekeza katika kila mradi mkubwa kuanzia mabibo hostel, udom, machinga complex, daraja la kigamboni, hospitali ya appolo india - tanzania na listi bado ni ndefu na pay back yake ni ya muda mrefu. Nyumba wanazojenga mtoni mtongani ya bei rahisi millioni 60 sasa kwa kipato cha mfanyakazi wa kawaida unaona kabisa hao wanojengewa hizo nyumba ni akina nani. Kupiga kelele haitusaidii sana tuombe tu listi ya wabunge watakaotutetea ktk hili regardless chama wanachotoka then waliobaki tuwamwage japo mpaka 2015 ifike wengi tutakuwa tushakufa. Hawa haki za binadamu wako wapi kununua hii kesi maana naona haki za msingi za binadamu zimekiukwa kwa kupitisha sheria bila mfanyakazi kuulizwa je anakubali au hataki. Jamani nashindwa hata niandike nini niache nini. Daa only made in tanzania!!!
 
Nimemsikiliza huyu mkurugenzi akiwa anaongea. Yaani ilibaki kidogo nipate hasara ya ka TV nilikokuwa nakaangalia kwa jirani. Kaonyesha wazi kuwa yeye sio mbunifu. Anasema eti hata wapi sijui huko hakuna fao la kujitoa. Mwambieni siku zote mambo mazuri ndio ya kuigwa. Wanatakiwa hao Ambao hawana hili fao awaalike waje waone tumewezaje sisi kuwa nalo kwa miaka yote na mifuko ikawa bado imara. Kwa akili yake kama ulaya au Amerika hawafanyi jambo fulani sisi hatutakiwi kulifanya?

kama vipi waige na ushoga basi maana hata marekani na uingereza imehalalishwa ndio tutajua kuwa kweli yote wayafanyayo wazungu ni mazuri na yanafaa kuigwa. Kama hilo la ushoga halifai basi hata hili la fao la kujitoa waliloiga baada ya kufilisika kwa hayo mashirika halifai ila ni wizi wa chukua chako mapema (ccm) wamebuni kuwanyonya raia wake.. Poor kikwete, Poor ccm, poor government they form..
 
Hiyo DAU kasema ukweli na ndivyo ilivyo na inapaswa kuwa hivyo, subiri mpaka ustaafu

Wanafiki na wapenda sifa hata kwetu wapo....ni bora ungesoma ni kwa nini watu wanapinga hii sheria ndo uje na hizi p..ba zako
 
...Job Security hapa Tanzania ni mbovu...hivyo si busara kujiringanisha na nchi nyingine juu ya mifuko ya ifadhi ya jamii hasa kwa upande wa fao la kujitoa wakati watu hawana uhalakika wa kudumu kwenye kibarua walau kwa miaka mitano.
 
GEPF ni pension fund. mbona ina fao la kujitoa pale unapomaliza mkataba wako kwa kazi uliyokuwa ukifanya?
 
Jaman GEPF mbona wanajitangaza kutoa fao la kujitoa? Hawa wapo nchi gani? kwanini wengine wasiige toka kwao?

Bahati mbaya kwa CCM kuruhusu mambo haya wakati huu!! Inazidisha chuki ya wafanyakazi dhidi ya serikali iliyopo madarakani, madhara yake ni kudorora kwa huduma kwa wananchi na hizi hasira tamati yake 2015.
 
Pamoja na udokita wake "amezoea kukopi na kupaste" na anawaza kuwa JAMBO ZURI HALIWEZI KUANZIA TZ wala mambo au taratibu zilizopo haziwezi kurekebishwa na Tanzania.
Kweli "uchungu wa mwana aujua mzazi".

Kweli kabisa. Inaonekana kabisa haelewi Watanzania wanataka nini. Ni dhahili hajui watanzania, ambao wengi wao hawana uhakika wakuishi kufikia miaka 55, hawataki kufananishwa na Wakenya wala Wamarekani na hivyo ni ushenzi kwake na PhD yake kuamini kuwa anao uwezo wakufikiri kwa niaba ya Watanzania wote. Angefanya research kidogo, kama ambavyo watu wengi wenye PhD original wanavyofanya (kwani wasomi waukweli huamini kuwa bila research, huwezi kufanya uamuzi uliokwenda shule), basi Dau huyu angepata kujua kuwa wapo Watanzania wengi wanaolazimika kuacha kazi ili wajitoe NSSF na wapate kumili nyumba zao na ndip waanze tena kazi. Vingenivyo, wangeweza kuja kumiliki nyumba wakiwa na miaka 60 na wameshachoka kuishi maisha ya dhiki yakupanga vyumba viwili na watoto watano. Dau funguka. Acha kufanya kazi za CCM. Utakufa pamoja na chama chako kinachokutuma kupeleka pesa zetu huko wanakotaka wao na kutuacha wenyewe tukitungiwa sheria zakishenzi.
 
Dau na waliokutuma na wanaokulinda unapofilisi michango ya wanachama kwa kuwekeza UDOM na daraja la Kigamboni, Tambua na kuelewa kwamba hakuna sehemu yeyote duniani michango ya wanachama inasaidia miradi ya serikali ambayo inapashwa kujengwa kwa kodi za nchi
 
Tatizo watanzania siasa tunaifanya kama ushabiki wa Simba na Yanga ukifika uchaguzi, we are not serious aisee, Siasa ni Maisha. Sasa tutulie tu CCM wafanye wanavyotaka, tunalialia nini?
 
Huyu jamaa kakopesha pesa zote serikalini, hana cha kuwapa wateja wake. He is buying time. Alichosahau ksema ni "hamna duniani kote ambapo serikali inakopa pesa zote mpaka kufilisi shirika" unapokopesha kwa masharti ya kipuuzi pesa haziwezi rudi. Hii ni sheria mama kwa shirika lolote la pesa linalojiheshimu.
 
Dr. Dau ana colonial mentality na probably madhara ya A.R.V feki
 
Basi wabunge wa upinzani watusaidie ili sheria iruhusu mwanachama kuhamishia michango yake kwenye mfuko anaoutaka ili wote tuhamie GEPF.
 
Huyu Dau amenikera nimemchukia na ukoo wangu wote, yani hii nchi mnyonge mnyongeni, kwavile wao wameshajilimbikizia mali wana zakuwatosha. Leo hii nisubiri miaka 55 naishi nyumba mbavu za mbwa, watoto hawakusoma, hiyo hela itanisaidia nini wakati huo, nguvu yenyewe sina wakati huo hata nguvu sina yakukimbizana na miradi,yani jamani nashindwa hata lakusema hakuna sababu yakujiandikisha tena kwa wanaoanza bora upokee chako chote kazi imeisha ndo mwisho basi.
 
Back
Top Bottom