Lager
JF-Expert Member
- Mar 4, 2019
- 395
- 1,085
Tangu tumekuwa katika hii sayari tumekuwa tukifikiri Kuna hichi kitu "Freewill!".
Ukweli mchungu ni huu,mazingira hayajatupa hiyo nafasi yakuwa na uhuru wa maamuzi ktk kila kitu ama kwa asilimia mia!.
Unayo nafasi ya kupumua ila hauna nafasi ya kupumua milele yote!,unayo nafasi ya kufa ila hauna nafasi ya kufufuka pale utakapotaka!.
Hata kula vivyohivyo!
Huo Uhuru wa kuamua tunachotaka ulishapangwa na mazingira ila hivi sasa yamebaki machaguo kutokana na vile ulivyo.
Kinachoniumiza kichwa ni aidha na hayo mazingira yalichagua tuwe hivi au nayenyewe hayakuwa huru katika kutuumba??.
Napata mashaka hata kuuweka uhuru tulionao ktk namba maana naona kama ktk uwanja huu wa boxing ktk freewill tumeshagalagazwa hata sisi hatujui!.
Unatafuta chakula ule ukijua hilo ni hitaji lako unalotakiwa kulitafuta,lakini ukweli ni kuwa system tulizowekewa ndio zinatutaka tule!.
Sina shida na hilo shida iliyopo ni sisi kufikiria tuna freewill lakini kumbe hatuna Uhuru wa moja kwa moja ila ni Uhuru Kama sub topic yaani UHURU halafu (uhuru),sisi tupo kwenye mabano.
Sipo hapa kwaajili ya kukashifu Uhuru tulionao au ambao hatuna ila kwaajili tu ya kukumbushana!.
Na ukweli mchungu ni kuwa pamoja na huu uhuru tulionao wa kwenye mabano bado pia unahitaji mabano ili mambo yaende sawia.
Ni akili halisi tu ndo inaweza kuelewa andiko hili na wala sio zile zilizokwenye mabano!,ktk haya maisha yetu hakikisha unakuwa na uhuru halisi wa kimazingira na sio ule wa kutaka kupumulia macho nawakati pua ipo.
Hata ulimwengu wetu unaongozwa na sheria na ndio maana wanadamu mpaka leo bado tunaufatilia ulimwengu ili tuweze kuzijua sheria hizo na tufumbuke zaidi.