Free will hakuna duniani haitotokea na endapo itakuja kutokea inaonyesha wazi wazi mungu anajichanganya anatunga sheria za ulimwengu ambazo zinapingana halafu anataka ziwe sawa
Kabla ya yote free will tunamaanisha uhuru wa nafsi katika kuchagua kufanya mema au mabaya swali je nani alileta mabaya?
Je Kati ya mtu na mabaya kipi kilianza kuumbwa?
Utakuja kuona mungu alianza kuumba Ubaya kabla ya kuumba mtu hivyo basi kwa vyovyote mambo mabaya lazima yawepo kwakuwa Ubaya ulianza kuumbwa rejea isaya " I form the light and creat darkeness ,I make peace and creat evil" isaya 45:7
Swali Je unamuhukumu vipi Yuda kwa kuchukua vipande vya dhahabu wakati tukio hilo lilishapangwa kuwa Yuda atakuja kumsaliti Yesu ?
Kwanini mungu aliumba uovu je alishindwa kuumba ulimwengu usiokuwa na mabaya na uovu ? Akaenda mbali zaidi akamuumba shetani wakati alijua huyu jamaa ataasi yaan akamuumba shetani na uovu na mabaya halafu anataka watu wawe wema ? Utakuja kuona hapa mungu anajichanganya huwezi kuanza kuumba mabaya na uovu na shetani juu halafu utegemee watu wawe wema
Niliwahi kuwa na maswali kama yako,
Nilipata majibu baada ya kusoma na kutafakari kitabu cha Genesis chapter one yote,
Nikagundua kuwa katika uumbaji mara sita MUNGU aliita aliyokua akiyaumba kuwa ni NJEMA
Na baada ya kukamilisha uumbaji MUNGU alitazama kila alichofanya kwa Mara ya saba akasema ni NJEMA SANA.
MUNGU HAKUUMBA UBAYA.
MUNGU aliumba Mtu na sio robot [emoji880]
Robot halina maamuzi, lemyewe hufanya kitu ilichoprogramiwa bila hata kureason.
Mungu alitupa "free will" na ipo hundred percent, ili tuamue tunachotaka kufanya.
Katika maamuzi yote tunayofanya duniani, yote yamebeba MACHAGUZI MAKUU MAWILI either KUCHAGUA KUMPENDEZA MUNGU au KUCHAGUA DHAMBI.
MUNGU HAKULAZIMISHI WW KUMFUATA AU KUMTII.
Ila anachofanya ni kukuambia ww faida za kumtii na consequences za kutokumii,
MAAMUZI YOTE YANAKUA JUU YAKO.
Alipo muumba Adam na Eva Eden aliwapa free will wao waaamue, either kula tunda au kutokula tunda.
Watu wengi wanaoquestion na kupinga doctrine ya "free will" huwa ni watu ambao tunaopenda kufanya vitu ambavyo n contrary na Mungu na tukifahamu consequences zake.
Na hizo consequences zinatufanya tuwe uncomfortable kwa sababu tunaona kama hatuna uhuru wa kuamua tunachokita ambacho n kumkataa Mungu bila kuface outcomes......