GE2025 Hakuna haja ya kusumbuka Oct 29.Kura haibadili chochote, na haihitajiki

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
WATANGANYIKA wenye akili October 29 tutatulia majumbani mwetu lkn pia wale waliopo maeneo salama waelekee mashambani kulima na wategemee neema ya mvua ALLAH ataileta amiin
 
..kwanini msumbuke wakati kura hazihitajiki? Mnapiga kura ili iweje?
Aliyekuweka kuwa determinant factor ya kuamua kuwa kura za watu hazihitajiki ni nani? Kwanza huo ujasiri wa kutuita wapumbavu unautoa wapi? Una maana kila asiyefikiri sawa na wewe ni mpumbavu? Huo ni ufinyu wa mawazo.
 
..fitina zimefanyika na kupelekea uchaguzi kuwa wa mtu mmoja, na chama kimoja. Ndio maana nasema hakuna haja ya kwenda kupiga kura. Hata kampeni hazikuwa na ulazima.
 
Ccm inashindana na nani haswa?

Wakati vyama vingine vyote ni proxy!
Wamewapa hela na magari na script, wakiamini huu ni mwaka 2000!
 
Naomba nikuulize mkuu hivi unavyosema unaenda kupiga kura kumchagua huyo raisi wako anashindana dhidi ya nani?
 
Yaani kuna mtu unaweza kumkuta amekaa mahali amevaa amependeza ukamuheshimu lakini akifungua tu mdomo unajuta Kwa Nini ulimuheshimu... Kuna watu humu ni heri wakae kimya tu pengine itasaidia maana kinachoendelea Kwa Sasa hapa nchini hakuna mwenye akili timamu asiyeelewa
 
SISIEMU kwakuwa wamejiunganisha na mifumo ya NIDA na NEC ,tayari tushatikiwa.
 
Naomba nikuulize mkuu hivi unavyosema unaenda kupiga kura kumchagua huyo raisi wako anashindana dhidi ya nani?
Wewe umeshajua ninayeenda kumpigia kura siyo? Kupiga kura ni hiari yangu, na wa kumpigia hiyo kura ni uchaguzi wangu. Wewe, au mtu mwingine yeyote hamna mamlaka ya kunipangia nimpigie nani kura. Hata nikipiga kura ya maruhani, bado ni hiari yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…