Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Kama kawa,
Ukiangalia nguvu iliyotumika jana kuzuia maandamano ya Chadema, nguvu hiyo ingetumika kuyalinda maandamano hayo badala ya kuyazuia!
Mada ya leo ni kuhusu haki, hakuna haki bila wajibu!, haki sio hisani ni stahiki inayopaswa kutolewa bila kuombwa. Haki ya kufanya mikutano na maandamano ni haki ya msingi ya vyama vya siasa, lakini pia vyama vina wajibu wa kufanya mikutano kwa amani na utulivu, wajibu wa kuhakiki amani na utulivu unakuwepo ni wajibu wa jeshi la Polisi, ndio maana vyama vinatakiwa kuiraifu Polisi mikutano na maandamano na ni jukumu la polisi kulinda amani kwenye mikutano hiyo na maandamano hayo, kitu cha ajabu kwenye maandamano ya jana, nguvu iliyotumika kuyazuia maandamano hayo ni kubwa ambayo ingetosha kabisa kuyalinda na Chadema wakaandamana kwa amani.
Haki sio hisani ya serikali, au jeshi la Polisi, haki ni stakihiki inayopaswa kutolewa bila kuombwa!. Haki haipaswi kuombwa, bali inapaswa kutolewa tuu, na isipotolewa haipaswi kuombwa bali inadaiwa, na ni katika kuidai huku sometimes hlazimika kugharimiwa kwa gharama za machozi, jasho na damu!.
Haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano na maandamano, ni haki ya msingi, iheshimiwe, waandamaji wana wajibu wa kuandamana kwa amani na kuitunza amani, utulivu na usalama, wakati huo huo, jeshi la Polisi lina wajibu wa kulinda amani, hivyo linapopata taarifa za kiiteligensia kuwa maandamano hayo yana malengo ya kificho ya "Samia Must Go", then jeshi la Polisi lina wajibu wa kuyazuia.
Leo naomba kurejejelea zile makala zangu za Ijue Katiba ya JMT kwa jicho la Mtunga Katiba, alidhamiria nini alipoweka kifungu fulani cha katiba. Ili tuweze kwenda sambasamba, naomba tukumbushane Katiba ni Nini?. Katiba ni kakitabu kadogo tuu chenye kurasa 113!. Kakitabu haka ndio kila kitu kuihusu Tanzania yetu, hakuna yeyote aliye juu ya Katiba.
Katiba ni ya Kazi Gani. Katiba ndio msingi Mkuu na muongozo wa uendeshaji wa nchi yetu, ambapo sheria zote, taratibu zote na kanuni zote, za kufanya kila jambo, lazima zitokane na katiba.
Misingi ya Katiba- Katiba yetu imeweka misingi mikuu 4 ya katiba ambayo ni uhuru, haki, udugu na amani. Misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu.
Hii maana yake, hii misingi mikuu 4 ya katiba yetu ambayo ni uhuru, haki, udugu na amani, Serikali, Bunge na Mahakama, zina wajibu wa kutekeleza, huu ni wajibu na sio hisani!. Tofauti ya wajibu na hisani, wajibu ni lazima utekelezwe, sio ombi, wakati hisani, ni huruma tuu unaweza ukatekeleza au usitekeleze kadri wewe unavyoona.
Turejee kwenye hii katiba, Katiba ni ya Nani? Katiba hii imetungwa na Bunge maalum kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia.
Hivyo kwa mujibu wa katiba hii, kitu muhimu kabisa kwa Taifa la Tanzania, ni watu!, Watanzania, hawa ndio wenye katiba!, katiba ni mali ya Watanzania. Ni watu hawa Watanzania, walioweka misingi mikuu minne ya katiba yetu, uhuru, haki, udugu na amani. Msingi mkuu wa kwanza wa katiba yetu ni uhuru, wa pili ni haki. Hivyo vitu vitu viwili vikuu vya katiba yetu ni uhuru na haki.
Katiba yetu ya mwaka 1977, unavyo vifungu kadhaa vya haki, kwenye vifungu hivyo, kunazo haki kuu za msingi. Haki kuu ni haki ya uraia, kuwa Mtanzania ndio haki kubwa kuliko zote, na Mtanzania ndicho kitu muhimu kuliko kitu chochochote ndani ya katiba yetu. Huyu mwananchi ndie mwenye nchi, mwenye katiba, anayemuajiri rais wa JMT kwa kura yake na kumlipa mshahara yeye na serikali yake, Bunge na Mahakama kwa kodi yake hivyo mwananchi ndie kila kitu!.
Kuanzia Ibara ya 5 hadi Ibara ya 30, haki mbalimbali zimetajwa na wajibu pia umetajwa, hapa nakutajia Ibara na haki yake
5. Haki ya kupiga kura.
11. Haki ya kufanya kazi, kupata elimu, na nyinginezo.
12. Usawa wa Binadamu. 13.Usawa mbele ya sheria.
14. Haki ya kuwa hai. 15.Haki ya uhuru wa mtu binafsi.
16. Haki ya faragha na ya usalama wa mtu.
17. Uhuru wa mtu kwenda atakako.
18.Uhuru wa maoni.
19. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo.
20. Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine.
21. Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.
22. Haki ya kufanya kazi. 23.Haki ya kumiliki mali. 24.Haki ya kupata ujira wa haki.
Pia katiba imeweka wajibu
25. Wajibu wa kushiriki kazini.
26. Wajibu wa kutii sheria za nchi.
27. Kulinda mali ya Umma.
28. Ulinzi wa taifa.
29. Haki na wajibu muhimu.
30. Mipaka kwa haki, uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu.
Baada ya haki hizo za msingi ndani ya katiba yetu, zikatungwa sheria na kutoa haki za mikusanyiko, haki za kufanya mikutano, haki za kuandamamana hadi haki za kufanya migomo.
Kufuatia vurugu za baadhi ya mikutano ya vyama, na maandamano kuleta taharuki kubwa nchini kutishia amani na utulivu, JPM, rais chuma wa Tanzania, bila kujali katiba inasema nini, alipiga marufuku mikutano ya siasa na maandamano kinyume cha katiba.
Rais Samia alipoingia, akaruhusu mikutano ya siasa, tukitaraji ni nderemo na vifijo nchi mzima!, kumbe sivyo , mikutano hii na maandamano imeanza tena kuleta tensions zisizo za lazima!, tusimfanya Rais Samia ajute kuruhusu mikutano na maandamano na wananchi waseme afadhali ya Magufuli.
Kwenye hili la kuzuiwa mikutano ya hadhara, kwa vyàma vya siasa kwa vile mikutano hiyo ya vyama vya siasa ni kitu ambacho kimeruhusiwa na katiba, kitendo kile cha kuzuia mikutano hii, hakikuwa sawa!, huu ilikuwa ni ukwiukwaji wa wazi kabisa wa katiba ya JMT mchana kweupe!.
Kufanya mikutano na maandamano ni miongoni mwa haki za vyama vya siasa zilizoainishwa na katiba, ila pia kwenye kila haki kuna wajibu!. hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu.
Kitu kama ni haki, then haki ni stahili sio hisani!, Je sisi Watanzania tutaendelèa kusubiri hadi lini wakati haki zetu na stahili zetu zikigeuzwa kuwa hisani?
Tena afadhali ya hili la haki ya mikutano ya siasa, limefanywa kwa utashi tuu kwa kutumia kauli tuu, yaani mikutano ilizuiliwa kwa kauli, na sasa imeruhusiwa kwa kauli, lakini kuna na haki nyingine mbili ambazo ndizo haki kuu za kiraia zilizotolewa na katiba yetu, haki za kuchagua na kuchaguliwa, nazo zimegeuzwa hisani!. Haki ya kuchagua yenyewe bado ipo, ila haki ya kuchaguliwa, haipo!, imenyofolewa na kufinyangwa finyangwa hivyo kuonekana kama ipo ila kiukweli ni haipo na mimi mwenyewe ni shahidi wa hili!
Watanzania tuendelee kuwa watu wa shukrani kwa kushukuru kwa yote, hata kama ni madogo ili tuweze kupatiwa makubwa, hivyo tuendelee kusema asante sana Mama Samia kwa a good political will la kuruhusu mikutano ya siasa, kwa utashi tuu hivyo vyama na Watanzania kukushukuru kwa hisani yako hii, tunakuomba tumia a political will kama hii hii kuwaruhusu Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa!
Haki ni stahiki sio hisani!, haki haiombwi na kutegemea hisani, wala haki haihitaji vikao, mikutano na majadiliano kuzijadili haki, na haki hauletewi kwenye kisahani cha chai kama hisani, fadhila au zawadi, haki ni stahiki inayopaswa kutolewa unconditional not as a favour, hisani au fadhila!
Haki is a right, inayopaswa kutolewa unconditional na isipotolewa, haiombwi, bali hudaiwa, na katika kuidai huku kukishindikana kuidai kwa amani na kisheria, ndipo nguvu hutumika kuipigania, but only pale inapobidi, na ni katika kuipigania huku sometimes machozi, jasho na damu huweza kumwagika!
Wito kwa vyama vya siasa, shime tufanye resiponsible politics, tufanye mikutano na maandamano responsibly kwa mujibu wa katiba, na serikali itemize wajibu wake responsibly kwa mujibu wa katiba. Nguvu iliyotumika kuyazuia maandamano ya juzi ya Chadema, ingeweza kutumika kuhakikisha wanaandamana kwa amani.
Mungu Mbariki Rais Samia aruhusu haki kama stahiki na sio haki kama hisani.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali