baz kaiza
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 14,971
- 18,641
Tuna tabia ya Kujidanganya Wenyewe kwamba hatuna matatizo ni kweli matatizo yapo tena makubwa Sasa hivi wale ambao walikua wanajificha kwenye amani kabla ya Maadamano wamekuja na hii ya kujificha kwenye kivuri cha Uharibifu wa vitu na mali. Unabaki unajiuliza nini kimepelekea kufika huko kilichopelekea kufika uko hakitakiwi kujadiliwa sasa kinachoendelea kujadiliwa ni uhalifu wa mali wizi ni sehemu gani ambayo inaweza kukusanya mkusanyiko wa watu mbalimbali kusiwepo wizi? Tunaona serikalini wizi ufisadi sio kwamba ni wote wanafanya au wanapenda ndo kama ilivyokua kwenye maandamano palipo na mkusanyiko wa watu wahalifu hawawezi kukosa wahalifu wako kila sehemu Tusikimbie kutimiza uwajibu wetu kwa kujificha kwenye viohoja baada ya hoja ya Msingi nini kimepelekea GenZ kuandamana basi hiyo ndo hoja kama GenZ kama wanaona mambo hayaendi sawa wekeni mambo sawa wazee wangu wa Chama mmesahau vijana ni Taifa la kesho vijana wanapigania kesho yao Tuwasikilize wanataka nini GenZ ni Vugu Vugu la nchi za Afrika sasa tumeona imewahi kutokea kwa wa waarabu ikaitwa Arabu spring tuache kutafuta mchawi wetu ni sisi wenyewe