Hakuna Kiongozi bora kama Rais wa TFF Wallace Karia, hivyo apewe Minne yake tena au atawale hata Milele TFF

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Amefanya Mambo mengi mazuri hasa katika kuleta Mandeleo ya Soka Tanzania

Katika Wagombea wote waliochukua Fomu Karia ni bora na anafaa kuliko wengine.

Tena ikiwezekana na Katiba ikiruhusu Wallace Karia aongoze Milele tu TFF kwani kafanya makubwa.

Ukiona Mtu anakubaliwa na GENTAMYCINE jua ni sahihi, mweledi na anafaa Kiutawala.

Ukiona Mtu yoyote au Timu fulani inamchukia Wallace Karia jua ni Wendawazimu watupu tu.

Rais Wallace Karia anakubalika na Wasomi wengi na Kutotakiwa na Wajinga wachache.

Namtakia kila Ia kheri Wallace Karia na asiwe na wasiwasi tunapoenda na ameshapita.

TFF si kwa kwenda kutafuta Followers Instagram au kutaka Kuuza tu Dawa za Kulevya.

Najitangaza rasmi JF kuwa Team Karia.
 
Watake , wasitake karia atapita tu.Anawatu wengi ,fitness kwenye uchumi icho lazima kitupeleke upande wake sie WANYONGE[emoji3][emoji3].Hao kina mayai waendelee kuchanganywa na chips tu na uchambuzi
 
Bora achaguliwe Oscar kuliko Karia! Kuna upande wanafaidika naye ndiyo mana wanampigia debe! Karia out .......
 
Karia alikuwa na bahati sana, kwenye utawala wake yamefanyika mambo makubwa yaliyokuwa nje ya uwezo wake kama kufuzu AFCON, Chan, na Simba SC kwenda klabu bingwa Afrika mara mbili.

Lakini yale yaliyokuwa ndani ya uwezo wake yote yamemshinda, viporo ligi kuu, waamuzi wabovu, ligi kukosa wadhamini wa maana muda mrefu mpaka Azam alipokuja kuokoa jahazi, kufungia viongozi wa soka vifungo virefu kwa makosa yanayostahili kulipa faini, n.k

Hivyo kumchagua Karia tena ni sawa na kuruhusu hayo majanga madogo madogo yaendelee kuiharibu ligi yetu na mpira wetu kwa ujumla.
 
Mafanikio ya Karia yamebebwa na nyakati tulizopitia/tunazopitia..chini ya utawala wake mengi yamefanyika kwa sapport ya serikali na hata upigaji uliogopwa kwa aina ya serikali ya mwendazake,pasi na hapo tff pangejaa harufu ya rushwa tupu..alichofanikiwa ni kuibeba Simba tu na si lingine
 
Karia alikuwa na bahati sana, kwenye utawala wake yamefanyika mambo makubwa yaliyokuwa nje ya uwezo wake kama kufuzu AFCON, Chan, na Simba SC kwenda klabu bingwa Afrika mara mbili.

Lakini yale yaliyokuwa ndani ya uwezo wake yote yamemshinda, viporo ligi kuu, waamuzi wabovu, ligi kukosa wadhamini wa maana muda mrefu mpaka Azam alipokuja kuokoa jahazi, kufungia viongozi wa soka vifungo virefu kwa makosa yanayostahili kulipa faini, n.k

Hivyo kumchagua Karia tena ni sawa na kuruhusu hayo majanga madogo madogo yaendelee kuiharibu ligi yetu na mpira wetu kwa ujumla.
Umeongea ukweli mtupu.Nakuunga mkono kwa asilimia mia.Tuko pamoja katika uchambuzi wako.
 
Tatizo letu wajumbe ambao ndio wapiga kura njaa tupu, wakitoka mikoani kwenda Tanga kupiga kura hawana nauli za kurudia makwao, mgombea atakaewapa hizo nauli ndio atashinda.
 
Kwa kipi alivholifanyia taifa kisoka?
1.Kukuza Soka la Wanawake

2.Kukuza Mapato Viwanjani

3.Taifa Stars Kufuzu AFCON

4.Kurejesha Nidhamu TFF

5.Kuvutia Wadhamini zaidi wa Ligi

6.FIFA Kuamini Tanzania kupitia Yeye

7.Kukuza zaidi Soka la Vjjana nchini

Anayemkataa au Kumchukia Wallace Karia akapimwe Akili upesi kama Mkude Muhimbili Hospitali au awahishwe Mirembe Dodoma.
 
Karia alikuwa na bahati sana, kwenye utawala wake yamefanyika mambo makubwa yaliyokuwa nje ya uwezo wake kama kufuzu AFCON, Chan, na Simba SC kwenda klabu bingwa Afrika mara mbili.

Lakini yale yaliyokuwa ndani ya uwezo wake yote yamemshinda, viporo ligi kuu, waamuzi wabovu, ligi kukosa wadhamini wa maana muda mrefu mpaka Azam alipokuja kuokoa jahazi, kufungia viongozi wa soka vifungo virefu kwa makosa yanayostahili kulipa faini, n.k

Hivyo kumchagua Karia tena ni sawa na kuruhusu hayo majanga madogo madogo yaendelee kuiharibu ligi yetu na mpira wetu kwa ujumla.
Ni Mwendawazimu tu ndiyo atamkataa Wallace Karia na hajajua Umuhimu wake katika Soka la Tanzania.
 
Back
Top Bottom