mkulimamiwa
JF-Expert Member
- Mar 4, 2025
- 2,591
- 5,315
Viongozi wa dini, ni waonesha njia, najiuliza, kwa sasa wanaonyesha njia Gani ikiwa uovu umetamalaki nchini? Watu wanapotea, wanatekwa na kuuwawa, lakini hatuoni kauli ya pamoja kama viongozi wawakilishi wa uwepo wa Mungu duniani?
Ni KWELI wanaitambua Nafasi Yao iliyowazi kwenye vitabu vitakatifu, kwamba wao ndio dira ya haki duniani? Na kwamba, kwa mjibu wa vitabu, wapo tayari kuilinda Imani hiyo hata kufa wakitetea haki ambayo Mungu ameiweka kwenye vitabu vyake?
Kuhubiri haki ni jambo moja na kuiishi haki ni jambo lingine pia
Mtu anayehubiri Haki na akaisimamia bila kuyumba Wala kutetereka, mtu huyo ndiyo Mungu hujivunia
Mapadiri, Wachungaji, Mashekhe na maasikofu, ni watu ambao vitabu vyao vinawaasa waihubiri haki na wao ndio wawe wa kwanza kuiishi, kuitetea na hata kuifia inapobidi
Viongozi Hawa wa Dini, badala ya kusimamia Yale ambayo Mungu amewaagiza, hawafanyi hayo, wamekuwa ni wenye kujipendekeza kwa wenye mamlaka hata pale haki za watu zinapokandamizwa, wengine wao wapo tayari kupewa kitu kidogo ili kuwasafisha wenye dhambi na wauwaji
Hawako tayari kusimamia haki Wala kukemea matendo maovu ya watawala ya watu wabaya kwa sababu ya kupenda fedha ya udharimu
Leo hii, Lissu ndio amekuwa dira ya viongozi wote wa dini, ni mtu ambaye Yuko tayari kumfia Kila mtu ilimradi Kila mtu apate haki ya kuishi, maana yake, badala ya viongozi wa Dini kuonesha njia ya kuioigania haki na kuifia pale inapobidi, Lissu sasa ndio amekuwa Shekhe, Padri, Asikofu na Mchungaji,
Viongozi wa dini, nyinyi ndo mmekuwa watu wa kutugawa kidini, wakati majukumu yenu ni kuwaunganisha watu na kuwaambia iliyokweli ya Mungu
Mnatugawanya kana kwamba ndilo agizo la huyo Mungu mnayemtumikia
Nawashauri Watanzania, bila kujali dini, tumuunge mkono Lissu kumtia moyo katika kuipambania haki
Mungu, ibariki TANZANIA