'Hakuna kitakachotuzuia' kuwaondoa Hamas, Netanyahu aiambia Marekani

Samson Ngomboli

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2019
Posts
1,598
Reaction score
2,710
EPACopyright: EPA

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pia ametoa taarifa baada ya kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken mjini Tel Aviv hii leo.

Alitaja shambulio baya la Jerusalem leo asubuhi, ambalo Hamas ilidai kuwa lilitekelezwa na wanachama wake. Netanyahu alisema ni "Hamas hao hao ambao wanajaribu kutuua kila mahali". "Nilimwambia: Tumeapa, nimeapa, kuwaondoa Hamas. Hakuna kitakachotuzuia."

Netanyahu anasema alimwambia Blinken kwamba Israel itaendeleza vita hadi ifikie "malengo matatu", ambayo anasema ni: "Kuwaachilia mateka wetu wote, kuwaondoa kabisa Hamas na kuhakikisha kwamba hakuna tishio kama hili litakalotokea tena kutoka Gaza."

BBC Swahili
 
Hakuna sasa kitachowazuia wapenda haki duniani na wao kuisambaratisha Tel Aviv.

Anaefikiri Wapalestina watamalizwa peke yao tu huyo ni mjinga.
 
Anatoa kaul za kishujaa mbele ya sponsa
 
Gaza ni kisehemu kidogo sana kama Kigamboni mpaka leo unaenda mwezi wa 3 wameishindwa kujua mateka walipo pamoja na Hamas wameishia kushambulia hospitali, shule, wanasema Hamas wamo humo wanauwa watoto na wanawake tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…