realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 3,925
- 8,853
Ni kweli kabisa tunakumbana na matatizo makubwa sana ambayo kwa namna moja ama nyingine likikufika unaweza ukaona kuwa sasa umekwisha.
Yani unaona kabisa hapa sitoboi hata iweje.
Ngoja nikuambie kitu.
Tatizo linapotokea wakati huo huwa linakuwa la moto sana kulingana na tatizo lenyewe.
Sasa kinachotakiwa kwako wewe ni kulipokea na kutulia kwani baada ya muda linapoa lenyewe na watu wanaendelea na mambo mengine.
Ukishalipata hilo tatizo usikae ukaanza kuwaza kwa nini mimi? Kwa nini mimi?
Unaweza ukaona wenzako wanacheka wanafurahi kumbe wao wana matatizo makubwa zaidi yako lakini hawakupi nafasi ya kuyajua.
Tulia na tatizo lako kunywa maji, sikiliza muziki unaoupenda huku ukitafakari namna ya kulitatua.
Hakuna kitu cha milele ni namna tu tunavyoyabeba.
Usiwaze sana na ukaamua kuchukua uamuzi mbaya kwa sababu ya Madeni, kazi,Ada na mambo kama hayo.
Tabasamu tena, hakuna kitu cha milele.