666 chata
JF-Expert Member
- Mar 14, 2013
- 1,700
- 3,921
1. Wakati flani nikifanya shughuli za kisheria ktk taasisi flani niliwai kukutana na mzee mmoja ambae kwa wakati huo alikua ana lala stendi ya mabus ubungo terminal, baada ya kutolewa kwenye nyumba yake kinguvu na watu wa bank kisa alishindwa kurejesha marejesho yake kwa wakati ambapo mpaka anatolewa alikua amebakiza Tshs milion tano tu. Kwa aibu familia aliihamishia kijijini kwao huko kusini na yeye kubakia hapa dar anapambania haki yake na hakua na kazi yoyote ile isipokua hio nyumba ndio alikua ana frame ambalo ndio lilikua duka linalo endeshea familia na hata mkopo aliokopa ulitumika kuliendeleza ilo duka ila mwisho wa siku ikawa ndio ivyo. (Tulipambana sana tukashinda, ila mpaka leo kesi inaendelea kwenye rufaa jamaa walikata rufaa na mzee hana makazi maalum).
2. Rafiki angu mmoja alipata ajali ya gari mwaka 2021 akalazwa hospital karibu miezi sita, akiwa kitandani alikua ana letewa wito wa kulipa madeni na samani za mahakamani, alikua ana changanyikiwa ananiambia "kinachoniuma sasa iv sio haya maumivu ya ajali niliyopata ila ni haya madeni, nachelewa kupona sababu ya simu za wadeni wangu". Alipata ajali wakati anadaiwa na watu kama sita na hakuna aliekua ana muelewa wanaona ajali ni story ya kutunga, askari polisi wamewai kufika kitandani alipolazwa kama mara mbili na wakaondoka, alikua haponi na anazidi kukonda sababu ni bill za hospitali na madeni ya watu vinapishana mlangoni.
3. Wakati flani nikakutana na mama ambae alikua ana mtaji wa milion 100 uliisha kisa mapenzi anavyodai, na baadae aka kopa milion 50 bank moja hapo posta na dhamana ikiwa ni nyumba yake aliyoijenga yeye mwenyewe hapo ukonga, wakati anafanya biashara alikua na ujauzito, akapata matatizo ya miguu, biashara yake ya kuuza viatu hapo karume ikawa na changamoto sana, mwisho vijana wake wakauza mzigo wote kwa bei ya hasara wakakimbilia south, wiki moja baada ya kujifungua ile benk ikaja na mabaunsa na madocument ambayo yanaonesha mnada ulifanyika muda tu so atoke kama alivyo na kila kitu akiache, kilichotokea alihifadhiwa na jirani yake hapo na akaona familia nyingine imehamia kwenye hio hio nyumba na wanavaa hadi kanga zake na wanatumia kila kilichokua ndani.
Madeni hayazoeleki na madeni hayaendeki kwa waganga, kama kutakua na uwezekano usikope kabisa au kopa ukiwa na plan A,B,C mpaka Q.
Sijajua wewe utakua una visa vipi vya madeni? au ulikwepa vp madeni? Tuambie tujifunze na tuchukue taadhari.