Hakuna kitu kibaya hapa duniani kama madeni

Wazee wa kukopa salary advance uzi unawahusu?

Kuna mtu nilimkopesha hela, tokea January mpaka dk hii ni dana dana mwa mwiii mpkaa nimechoka.
Laki na nusu naanzaje tu kuipotezea? Kwa hela zipi nilizo nazo!! Nimempa last chance ya mwezi huu, nao unaelekea kuisha yuko kimya aibu haoni. Naumia basi tu 🥺🥺

Nyieee mkikope na mjue kulipa, nimejiambia mimi tena kukopesha? Labda nikuone hapo unaelekea kufariki
Achana nae huyo baby. Ngoja nikutumie laki tano unywe supu.
 
Halafu utamsikia mchungaji sijui wanajiita wenyewe “mtumishi wa Mungu” anahubiri ameinua mkono juu anasema “wewe unaedaiwa madeni yako yanaenda kuisha sasa” jitu na akili zake linaitika amen ukimuuliza ile 700K ya jamaa uliyokopaga mpaka sasa umerudisha bei gani anakwambia sijarudisha hata mia.

Madeni ni mabaya kaka yangu 2012 hawa access bank waliuza nyumba yake pale Mburahati kwa deni la Tsh 1.7mill na jela wakataka kumtia.
Tena huyo mwenye Madeni,Anatoa bonge la Sadaka.
 
Majembe Auction Mart
Katika orodha ya maswali kwenye usaili ni kama ifuatavyo!
1. Ulishawahi kutumia bangi?
2. Ulishawahi kuona maiti?
3. Ulishawahi kumpasua mtu na chupa?
4. Unaweza kunywa damu mbichi?
5. Unajua wakopaji wasiyolipa madeni kwa wakati ndiyo waliowafanya wananchi wa chini ukiwemo wewe muomba ajira kukosa hela?
6. Thibitisha ukatili wako (hapa ndipo unatakiwa umpasue paka utumbo umle au ujipasue kidogo halafu unywe damu yako) ukifuzu kazi umepata!
KITUO KINACHOFUATA SITE NDIPO ATAJUA HAJUI! Hata ukikutwa na mimba unataka kujifungua wanakutimua, ukutwe na dripu wanakusogeza pembeni ufe vizuri! Kazi kazi! DAWA NI MOJA TU USIKOPE AU LIPA KWA WAKATI!
 
Mkuu, kama hauna madeni basi wewe ndio tatizo. Yaani hauaminiki na imefikia hatua haukopesheki...🙄
 
Madeni ni balaa mi kukopa siwezi mtanisamehe sikumbuki lin nilikopa hata miaka 13 nyuma sijawai kukopa kutokan imani na asili yetu kukopa ni laana
Chuo ni kula mihogo ndo bajeti iliyopo natumia kilicho changu sina tamaa labda bodi ya mikop ndo namalizana nao hivi punde
 
1. Wakati flani nikifanya shughuli za kisheria ktk taasisi flani niliwai kukutana na mzee mmoja ambae kwa wakati huo alikua ana lala stendi ya mabus ubungo terminal, baada ya kutolewa kwenye nyumba yake kinguvu na watu wa bank kisa alishindwa kurejesha marejesho yake kwa wakati ambapo mpaka anatolewa alikua amebakiza Tshs milion tano tu. Kwa aibu familia aliihamishia kijijini kwao huko kusini na yeye kubakia hapa dar anapambania haki yake na hakua na kazi yoyote ile isipokua hio nyumba ndio alikua ana frame ambalo ndio lilikua duka linalo endeshea familia na hata mkopo aliokopa ulitumika kuliendeleza ilo duka ila mwisho wa siku ikawa ndio ivyo. (Tulipambana sana tukashinda, ila mpaka leo kesi inaendelea kwenye rufaa jamaa walikata rufaa na mzee hana makazi maalum).

2. Rafiki angu mmoja alipata ajali ya gari mwaka 2021 akalazwa hospital karibu miezi sita, akiwa kitandani alikua ana letewa wito wa kulipa madeni na samani za mahakamani, alikua ana changanyikiwa ananiambia "kinachoniuma sasa iv sio haya maumivu ya ajali niliyopata ila ni haya madeni, nachelewa kupona sababu ya simu za wadeni wangu". Alipata ajali wakati anadaiwa na watu kama sita na hakuna aliekua ana muelewa wanaona ajali ni story ya kutunga, askari polisi wamewai kufika kitandani alipolazwa kama mara mbili na wakaondoka, alikua haponi na anazidi kukonda sababu ni bill za hospitali na madeni ya watu vinapishana mlangoni.

3. Wakati flani nikakutana na mama ambae alikua ana mtaji wa milion 100 uliisha kisa mapenzi anavyodai, na baadae aka kopa milion 50 bank moja hapo posta na dhamana ikiwa ni nyumba yake aliyoijenga yeye mwenyewe hapo ukonga, wakati anafanya biashara alikua na ujauzito, akapata matatizo ya miguu, biashara yake ya kuuza viatu hapo karume ikawa na changamoto sana, mwisho vijana wake wakauza mzigo wote kwa bei ya hasara wakakimbilia south, wiki moja baada ya kujifungua ile benk ikaja na mabaunsa na madocument ambayo yanaonesha mnada ulifanyika muda tu so atoke kama alivyo na kila kitu akiache, kilichotokea alihifadhiwa na jirani yake hapo na akaona familia nyingine imehamia kwenye hio hio nyumba na wanavaa hadi kanga zake na wanatumia kila kilichokua ndani.

Madeni hayazoeleki na madeni hayaendeki kwa waganga, kama kutakua na uwezekano usikope kabisa au kopa ukiwa na plan A,B,C mpaka Q.

Sijajua wewe utakua una visa vipi vya madeni? au ulikwepa vp madeni? Tuambie tujifunze na tuchukue taadhari.
Tatizo la benki zetu hapa zinazo kopesha sio kwamba zinalenga kukunyanyua kiuchumi ila zinalenga kuchukua mali zako, pia ma dalali wa benki wanashawishi watu kwa kuwambia uongo kuhusu huo mkopo pia riba ziko juu.
 
YONO auction ili ufanye kazi kwao sifa kuu uwe na roho mbaya!

Na hiyo Roho mbaya unatakiwa uithibitishe kwenye INTERVIEW!
unaweza kwenda na kuku ukamchana chana na mikono au unaweza kumkamata paka ukamla nyama mbichi...
Au unaweza piga kichwa ukutani, damu ikitoka unajilamba!

Baada ya hapo kituo kinachofuata ni kwa mteja ndipo atajua hajui

Kukopa sherehe kulipa msiba

Unachukua mkopo wa 100mil unanunulia nyumba au gari!
Wakija kuchukua nyumba yao sioni kama kuna tatizo MAANA ULIKUWA HUNA KITU ndo maana ukakopa,sasa wanachukua kukuacha ulivyokuwa sioni kama ni shida!
KOPA KUJAZIA PALIPOPELEA, SIYO UNAKOPA KWA KUDANGANYA VIELELEZO
😂😂😂😂😂🙌🏾
 
Madeni madeni...

Mbona niliuza Kiwanja cha 20/20 Chenye pagara La vyumba vitano ..matofali ya kuchoma 1.5 milioni.

Yote Maisha lakini..

Inaitwa kutatua tatizo KWA kutengeneza tatizo Kubwa zaidi..
 
Huwezi kuwa tajiri bila madeni....
Tofautisha madeni na mikopo ..
Inayolipika .. mikopo itolewayo kulingana na collateral.. mikopo KWA ajili ya Biashara inayoendelea ...
Mikopo KWA Mtu aliyeko kwenye mzunguko wa Biashara ... Mikopo KWA Corporation/kampuni ambayo mali za kampuni haziusishwi na mali binafsi ...
 
Wazee wa kukopa salary advance uzi unawahusu?

Kuna mtu nilimkopesha hela, tokea January mpaka dk hii ni dana dana mwa mwiii mpkaa nimechoka.
Laki na nusu naanzaje tu kuipotezea? Kwa hela zipi nilizo nazo!! Nimempa last chance ya mwezi huu, nao unaelekea kuisha yuko kimya aibu haoni. Naumia basi tu [emoji3064][emoji3064]

Nyieee mkikope na mjue kulipa, nimejiambia mimi tena kukopesha? Labda nikuone hapo unaelekea kufariki
Nyakati hazilingani dada nawewe one day unaweza kujikuta unakopa!
 
1. Wakati flani nikifanya shughuli za kisheria ktk taasisi flani niliwai kukutana na mzee mmoja ambae kwa wakati huo alikua ana lala stendi ya mabus ubungo terminal, baada ya kutolewa kwenye nyumba yake kinguvu na watu wa bank kisa alishindwa kurejesha marejesho yake kwa wakati ambapo mpaka anatolewa alikua amebakiza Tshs milion tano tu. Kwa aibu familia aliihamishia kijijini kwao huko kusini na yeye kubakia hapa dar anapambania haki yake na hakua na kazi yoyote ile isipokua hio nyumba ndio alikua ana frame ambalo ndio lilikua duka linalo endeshea familia na hata mkopo aliokopa ulitumika kuliendeleza ilo duka ila mwisho wa siku ikawa ndio ivyo. (Tulipambana sana tukashinda, ila mpaka leo kesi inaendelea kwenye rufaa jamaa walikata rufaa na mzee hana makazi maalum).

2. Rafiki angu mmoja alipata ajali ya gari mwaka 2021 akalazwa hospital karibu miezi sita, akiwa kitandani alikua ana letewa wito wa kulipa madeni na samani za mahakamani, alikua ana changanyikiwa ananiambia "kinachoniuma sasa iv sio haya maumivu ya ajali niliyopata ila ni haya madeni, nachelewa kupona sababu ya simu za wadeni wangu". Alipata ajali wakati anadaiwa na watu kama sita na hakuna aliekua ana muelewa wanaona ajali ni story ya kutunga, askari polisi wamewai kufika kitandani alipolazwa kama mara mbili na wakaondoka, alikua haponi na anazidi kukonda sababu ni bill za hospitali na madeni ya watu vinapishana mlangoni.

3. Wakati flani nikakutana na mama ambae alikua ana mtaji wa milion 100 uliisha kisa mapenzi anavyodai, na baadae aka kopa milion 50 bank moja hapo posta na dhamana ikiwa ni nyumba yake aliyoijenga yeye mwenyewe hapo ukonga, wakati anafanya biashara alikua na ujauzito, akapata matatizo ya miguu, biashara yake ya kuuza viatu hapo karume ikawa na changamoto sana, mwisho vijana wake wakauza mzigo wote kwa bei ya hasara wakakimbilia south, wiki moja baada ya kujifungua ile benk ikaja na mabaunsa na madocument ambayo yanaonesha mnada ulifanyika muda tu so atoke kama alivyo na kila kitu akiache, kilichotokea alihifadhiwa na jirani yake hapo na akaona familia nyingine imehamia kwenye hio hio nyumba na wanavaa hadi kanga zake na wanatumia kila kilichokua ndani.

Madeni hayazoeleki na madeni hayaendeki kwa waganga, kama kutakua na uwezekano usikope kabisa au kopa ukiwa na plan A,B,C mpaka Q.

Sijajua wewe utakua una visa vipi vya madeni? au ulikwepa vp madeni? Tuambie tujifunze na tuchukue taadhari.
Madeni yanakuaibisha na kuidhalilisha familia yako nakukufanya kuwa masikini wa kutupwa, siku zote mimi kanuni yangu ni moja usikope dhaidi ya 20% ya pato lako kwa mwezi.
 
kutokomeza mikopo na madeni inabidi tuanzie huku

3032699_IMG-20211214-WA0000.jpg
 
Mikopo mibaya sana..nakumbuka 2018 nilipitia kipindi kigumu nikajikuta naingia kwenye madeni..aisee kuna watu wanajua kudai ..siku nayamaliza niliapa sintokuja kukopa tena..labda nikizidiwa sana..kama umeolewa watakuja kwa mmeo..wataenda kwa wazazi wako..watakuja na ofisini..kuna marafiki zangu kadhaa ilibidi waache kazi Ili kukimbia wadeni..na Wengine walifukuzwa kazi kwa sababu ya wadeni kuja kushtaki ofisini..deni ni adhabu ...huna amani huna furahaa..maisha hayendi na unajikuta unafanyia watu kazi..
Mwisho wa mwezi ukifika hela yote inaishia kwenye madeni..Ili ku survive unajikuta unakopa tena...
 
YONO auction ili ufanye kazi kwao sifa kuu uwe na roho mbaya!

Na hiyo Roho mbaya unatakiwa uithibitishe kwenye INTERVIEW!
unaweza kwenda na kuku ukamchana chana na mikono au unaweza kumkamata paka ukamla nyama mbichi...
Au unaweza piga kichwa ukutani, damu ikitoka unajilamba!

Baada ya hapo kituo kinachofuata ni kwa mteja ndipo atajua hajui

Kukopa sherehe kulipa msiba

Unachukua mkopo wa 100mil unanunulia nyumba au gari!
Wakija kuchukua nyumba yao sioni kama kuna tatizo MAANA ULIKUWA HUNA KITU ndo maana ukakopa,sasa wanachukua kukuacha ulivyokuwa sioni kama ni shida!
KOPA KUJAZIA PALIPOPELEA, SIYO UNAKOPA KWA KUDANGANYA VIELELEZO
unanichekesha na junijumbusha japo ilikua mazingira ya kazi ila yanafana na haya boss alifika ktk tuliokua tunaitaji kazi,,swali namba moja anataka kazi ya kusimamia site unafanya ibada or unatumia vilevi jibu kalibia wote wafanya
na vilevi awatumii ikafika zamu yangu muda huo nishawaka asubuhi nishavurugwa alivyouliza nikamjibu mkuu me sijui lini nilifanya ibada labda zile za mazishi huwa nauzuria akicheka sana,,sijakaa sawa kitu kikanidondoka ktk jacket alicheka sana nikachaguliwa nikapige kazi .ila hii simulizi nikipata muda nitaileta wakuuu
 
Back
Top Bottom