Niliwahi mwambia mdogo wangu wakike miaka ya nyuma, gauni halijakupendeza, akanuna na kutoka hivyo hivyo, kufika alikokuwa anaenda mashoga zake wakamuuliza vipi shosti hukutokea home nini? akawauliza kwann? wakamjibu mbona upo normal sana hujadamshi. Akaelewa kuwa ni kweli hakuwa amependeza, aliporudi akaniambia. Nikanyamaza.
Siku nyingine akanifuata na mchoro wa gauni anataka akashone, nikamwambia huu umekaa kibibi sasa, ngoja nikutafutie mshono online, hakungoja, huyooo kwa fundi, baada ya wiki akarudi na gauni lake, kulivaa, mama akamwambia loooooooo yaani kitenge kizuri umeenda kukiharibu mwanangu, ndo umeshona kituko gani hicho. Akaniangalia, nikafumba macho.
Kuanzia siku hiyo, akawa akija na jambo lake, mi naunga mkono hoja tu, mpaka akajua kuwa bro hana time tena na mimi, akaamua kujishusha na kuacha ujuaji, ikawa akiomba ushauri kama yupo sahihi namwambia, kama kabugi namwambia na anachukua ushauri.
So tuendelee kujikinga wenyewe mpaka hapo watakapoona kuwa sisi nasi watu sio mifugo.