Hakuna mabadiliko ndani ya club ya Simba, msidanganyike

Hakuna mabadiliko ndani ya club ya Simba, msidanganyike

Maendeleo ya simba hayapingwi kwa hoja nyepesi namna hiyo.Timu haiwezi akaendeshwa kwa kutegemea makapi ya wachezaji.Tunamtaka Mo atuletee wachezaji wenye hadhi ya Jina la Simba.Hilo linawezekana kama tukifanikiwa kufungua milango ya uwekezaji.Hakuna asiyetaka faida,hivyo hata Mo akifaidika klub nayo itafaidika hasa kwa kuongeza mapato na washabiki kwa matokeo mazuri.Simba ilitakiwa iwe kama TP Mazembe kwa ukongwe wake,lakini leo haina hata pesa ya kusajili wenye uwezo wa level za Mazembe.
 
Yuko kwa ajili ya kupata faida. Ebu fuatilieni viwanda vyake anavyoviendesha anaviendeshaje ndio mtapata jibu.
 
Kwani Mkodisho FC uko nafasi ya ngapi..!? ligi kuu
Uko pale ukiwa unajua kabisa mwenye nafasi yake anakuja....

Kulikuwa na gape la alama nane.. 8

Zikapungua zikawa alama tano.. 5

Zikapungua zikawa alama mbili.. 2

Mlivyoona hii pace ya wanajangwani mkaanza kuweweseka na kuibuka migogoro ya mishahara.

Mashukuru Mungu mzunguko ukawa unafika tamati.. [emoji23]
 
Mtu kama hakubaliani na mwenendo Wa simba ahamie lipuli....tuachieni timu yetu Alaaah!!!
 
Vijana wa siku hizi tabia zao zinafanana wanaombea wazazi wao wafe wauze mali za urithi halafu baada ya muda wanakuwa choka mbaya ukweli hawa wazee mnaowadharau ndio waliwafanya nyinyi muipende simba wengine mnatamba simba ilikuwa klab ya kwanza kufika nusu fainali ya afrika oh simba ilimfunga yanga 6 bila kama ukiwasikiliza kwa makini wadhamini wa simba walikuwa wanazungumzia taratibu zifatwe kwanza walitaka uhakiki wa wanachama ufanyike, pili walitaka wanachama waeleweshwe kuhusu mfumo wa hisa ila kwa sababu watu wamesikia kuna bilioni 20wamesahau taratibu zote.kabla ya kuuza hisa ilitakiwa ifanyike tathimini ya thamani ya simba, tunapoongelea thamani ya simba hatuongelei majengo au uwanja wao wa bunju bali ni idadi ya mashabiki walionao.GHivi kuna watu wamemwuliza mo kwanini aliuza african lyon au nini kilimfanya akaacha kudhamini singida united yule ni mfanyabiashara kinachompeleka sio mapenzi bali ni jinsi gani atajitanua kibiashara.Iwapo ingefanyika tathimini ya kina na thamani ya simba ikajulikana ni wazi walitakiwa watoke wanunuzi tofauti washindanishwe na kila mtu angekuja na bei yake mwenye bei nzuri na ambaye anajulikana ni simba ndiye angepewa nafasi ila huu mchakato umeendeshwa kihuni sababu viongozi wa simba ni wahuni ndio maana pesa za mauzo ya wachezaji hazieleweki ziko wapi na pesa hizohizo ndio zinawafunga watu midomo
 
Back
Top Bottom