Pre GE2025 Hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika kwenye haki ya wafungwa kupiga kura, Makalla amepotosha!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
No reforms no election
 
Mbona kwa wazanzibar wenzake hana kiburi?
 
Ahsante Kaka. Umesema mnatakiwa kuwa upande wa kweli. Kwa mtazamo wako hoja za Lissu kuhusu chaguzi zetu na ubovu wa Katiba yetu ni kweli au si kweli? Kama ni kweli, kwa nini usichague upande wa upinzani?
Pia umesema wanahabari hamtakiwi kuegemea upande wowote. Hapa sidhani kama umesema kweli, kwa sababu wanahabari wengi hamzitangazi hoja za wapinzani kwa upana wake pia tumeona mara kadhaa matukio ya wapinzani kwenye Tv yakikatishwa.
Mwisho Ccm/Serikali ni lidude likubwa sana lenye nguvu nyingi sana, linapambana na wapinzani wenye nguvu dhaifu. Hamuoni kama nyinyi wanahabari kuwa Neutral ni kuuonea upinzani? Hata Wlm Nyerere aliwahi kusema "mwenye nguvu sana akipambana na dhaifu sana halafu wewe ukasema upo Neutral utakuwa unakosea"
 
Ahsante Kaka.
Mkuu Bra, Bra-joe ,kwanza asante kwa objectivity yako kwasababu hii jf ya kisasa,kupata watu objective ni wakutafuta kwa tochi!
Umesema mnatakiwa kuwa upande wa kweli. Kwa mtazamo wako hoja za Lissu kuhusu chaguzi zetu na ubovu wa Katiba yetu ni kweli au si kweli?
Ni kweli kabisa,Lissu, Chadema na wapinzani, wana hoja ya msingi kabisa kuhusu ubovu wa katiba yetu na udhaifu wa chaguzi zetu, hivyo hitaji la reforms,ni hitaji la msingi sana!。
Kama ni kweli, kwa nini usichague upande wa upinzani?
japo madai ya upinzani ni madai ya msingi,the approach ya kudai is a wrong approach,huwezi kusema no election!,rais mwenyewe wa nchi hawezi kusema no election!,who are you useme no election?!。
Pia umesema wanahabari hamtakiwi kuegemea upande wowote. Hapa sidhani kama umesema kweli, kwa sababu wanahabari wengi hamzitangazi hoja za wapinzani kwa upana wake pia tumeona mara kadhaa matukio ya wapinzani kwenye Tv yakikatishwa.
hapo kuna matatizo both ways,media isiyotenda haki kwa wapinzani,na wapinzani wasiojitambua na kufanya siasa za hadaa,utopian politics。
Mwisho Ccm/Serikali ni lidude likubwa sana lenye nguvu nyingi sana, linapambana na wapinzani wenye nguvu dhaifu. Hamuoni kama nyinyi wanahabari kuwa Neutral ni kuuonea upinzani?
hapana,
Hata Wlm Nyerere aliwahi kusema "mwenye nguvu sana akipambana na dhaifu sana halafu wewe ukasema upo Neutral utakuwa unakosea"
huu ni mtazamo wake。
P
 
Kaka nataka kukuelewa lakini akili yangu inagoma. Nadhani utakubaliana na Mimi kwamba Adui mkubwa anayehatarisha Amani ya Taifa letu ni mfumo mbaya wa chaguzi zetu na ubovu wa katiba yetu.
Umekuta watu wanapambana na huyu Adui kwa manufaa ya Taifa, unawaambia sawa pambaneni naye tuko pamoja. halafu wewe unaanza kuwabeza kwa namna wanavyopambana na Adui. Hii haijakaa sawa.
Kwa kuwa wote tunakubaliana Adui yetu ni mmoja basi hatunabudi kuungana, kupigana kwa pamoja kila mtu na silaha yake kuhakikisha Adui (anakufa) anaondoka Nchini kwetu.
Kama unavyojua vita, hapa kutakuwa na upotevu mkubwa wa Maisha, mali, Maslahi na hata wengine kupata ulemavu wa kudumu. Hapa ndipo ninapouona ugumu wa Watanzania wengi kupambana na Adui yetu huyu.
Tupambane kwa kesho ya Taiga letu.
 
Pokea maua yako Mkuu.
 
Chawa chawa yaani siku hizi ni mwendo wa kububujikwa machozi ya huzuni tu... kila mnapogeuka mnalabuliwa... lazima mkae mguu sawa saivi
My lady,
chukua hayo mambo matatu ni muhimu sana kuyazingatia kuelekea uchaguzi mkuu wa October mwaka huu 2025, ukamueleze na mwenyekiti wa chama chako na itapendeza sana,

huna haja ya kubabaika sana 🐒
 
Sasa rais atasemaje no election wkt yy ndio mnufaika wa election yenyewe pascally mbona unazeeka vibaya hivyo
 
Makalla mzee wa hovyo sana CPA chawa
 
Kw
Kuwa mkweli, kwenye mkutano wa media na TAL, uneutral wako uliuweka mfukoni na ukaonesha sura yako halisi kwamba upo upande gani!

Maswali yako yote uliyojenga kumuuliza TAL, tayari yalikuwa yashajadiliwa sana humu JF na kupatiwa majibu kwa ufasaha kabisa kwamba Ssh kwenda Nairobi kumuona majeruhi haikuwa safari iliyopangwa, bali alipitia kwa kujibaraguza, kujikosha na 'kuzuga'.

Halafu la kumwachia Mbowe haikuwa hisani bali ni takwa la kisheria kwa sababu ilikuwa ni kesi ya 'kubumba', yote hayo wanaJf tulikuwa tushayafanyia kazi.

Kuibua maswali ya namna hiyo ambayo majibu yake halisi ulikuwa nayo, kwanza hadhira ilikuona kuwa wewe ni chawa na muumini wa mi5 tena kindaki ndaki.

Wanyumbani uliboa na ulituchosha sana mashabiki zako ujue!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…