Pre GE2025 Hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika kwenye haki ya wafungwa kupiga kura, Makalla amepotosha!

Pre GE2025 Hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika kwenye haki ya wafungwa kupiga kura, Makalla amepotosha!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hakuna haja ya kubabaika wala kumbwelambwela kuelekea uchaguzi mkuu wa kihistoria Oct mwaka huu 2025,

Mambo matatu muhimu yafuatayo ya kisheria kuhusu uchaguzi yalilifanyiwa marekebisho na bunge.

1. Hapatakua na mgombea kupita bila kupingwa, kila mgombea ni Lazima apigiwe kura.

2. Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya hawatakua wasimamizi wa uchaguzi, badala yake watumishi waandamizi wa umma watawajibika kusimamia jukumu hilo zito na muhimu sana la kidemokrasia nchini.

3. Wafungwa wote wa chini ya miezi sita, watapata fursa ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na watashiriki zoezi la kupiga kura sambamba na wapiga kura wengine.

Sote tushiriki kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura litakalo anza March 17 katika mkoa wa Dar es salaam.
Usipange kukosa kupiga kura 🐒
No reforms no election
 
Mkuu Cute Wife ,ubarikiwe sana kwa elimu hii!,mimi nimepandisha humu mabandiko zaidi ya 100 kuomba mabadoliko ya katiba,kurejesha haki ndani ya katiba yetu!。

Kwa vile,tumeomba sana,kupitia maandiko, sauti, vipindi vya redio na TV, she did nothing!,before the last final,attempt,nafanya utafiti if she is innocent genuine,kama ni kweli hajui,tutamsamehe,
Inawezekana ni Kiburi na Jeuri or Real Busy? Wasaidizi wake hawajamwambia ukweli wa ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?,Tufanye nini kupata Haki? lakini kama ukweli anajua ila ni anatufanyia kiburi tuu na jeuri ya madaraka na mamlaka, then。。。!

P
Mbona kwa wazanzibar wenzake hana kiburi?
 
Ni inaonekana ni kama,sijawahi kuegemea upande wa serikali。

kwa mujibu wa fani yetu,sisi。media ni non partisan, tunapaswa kuwa neutral wakati wote.

media tukaa upande wa wakweli,kama wakandamizaji ni wa kweli,tunasimama nao!。

Nimekusikia。
P
Ahsante Kaka. Umesema mnatakiwa kuwa upande wa kweli. Kwa mtazamo wako hoja za Lissu kuhusu chaguzi zetu na ubovu wa Katiba yetu ni kweli au si kweli? Kama ni kweli, kwa nini usichague upande wa upinzani?
Pia umesema wanahabari hamtakiwi kuegemea upande wowote. Hapa sidhani kama umesema kweli, kwa sababu wanahabari wengi hamzitangazi hoja za wapinzani kwa upana wake pia tumeona mara kadhaa matukio ya wapinzani kwenye Tv yakikatishwa.
Mwisho Ccm/Serikali ni lidude likubwa sana lenye nguvu nyingi sana, linapambana na wapinzani wenye nguvu dhaifu. Hamuoni kama nyinyi wanahabari kuwa Neutral ni kuuonea upinzani? Hata Wlm Nyerere aliwahi kusema "mwenye nguvu sana akipambana na dhaifu sana halafu wewe ukasema upo Neutral utakuwa unakosea"
 
Ahsante Kaka.
Mkuu Bra, Bra-joe ,kwanza asante kwa objectivity yako kwasababu hii jf ya kisasa,kupata watu objective ni wakutafuta kwa tochi!
Umesema mnatakiwa kuwa upande wa kweli. Kwa mtazamo wako hoja za Lissu kuhusu chaguzi zetu na ubovu wa Katiba yetu ni kweli au si kweli?
Ni kweli kabisa,Lissu, Chadema na wapinzani, wana hoja ya msingi kabisa kuhusu ubovu wa katiba yetu na udhaifu wa chaguzi zetu, hivyo hitaji la reforms,ni hitaji la msingi sana!。
Kama ni kweli, kwa nini usichague upande wa upinzani?
japo madai ya upinzani ni madai ya msingi,the approach ya kudai is a wrong approach,huwezi kusema no election!,rais mwenyewe wa nchi hawezi kusema no election!,who are you useme no election?!。
Pia umesema wanahabari hamtakiwi kuegemea upande wowote. Hapa sidhani kama umesema kweli, kwa sababu wanahabari wengi hamzitangazi hoja za wapinzani kwa upana wake pia tumeona mara kadhaa matukio ya wapinzani kwenye Tv yakikatishwa.
hapo kuna matatizo both ways,media isiyotenda haki kwa wapinzani,na wapinzani wasiojitambua na kufanya siasa za hadaa,utopian politics。
Mwisho Ccm/Serikali ni lidude likubwa sana lenye nguvu nyingi sana, linapambana na wapinzani wenye nguvu dhaifu. Hamuoni kama nyinyi wanahabari kuwa Neutral ni kuuonea upinzani?
hapana,
Hata Wlm Nyerere aliwahi kusema "mwenye nguvu sana akipambana na dhaifu sana halafu wewe ukasema upo Neutral utakuwa unakosea"
huu ni mtazamo wake。
P
 
Mkuu Bra, Bra-joe ,kwanza asante kwa objectivity yako kwasababu hii jf ya kisasa,kupata watu objective ni wakutafuta kwa tochi!

Ni kweli kabisa,Lissu, Chadema na wapinzani, wana hoja ya msingi kabisa kuhusu ubovu wa katiba yetu na udhaifu wa chaguzi zetu, hivyo hitaji la reforms,ni hitaji la msingi sana!。

japo madai ya upinzani ni madai ya msingi,the approach ya kudai is a wrong approach,huwezi kusema no election!,rais mwenyewe wa nchi hawezi kusema no election!,who are you useme no election?!。

hapo kuna matatizo both ways,media isiyotenda haki kwa wapinzani,na wapinzani wasiojitambua na kufanya siasa za hadaa,utopian politics。

hapana,

huu ni mtazamo wake。
P
Kaka nataka kukuelewa lakini akili yangu inagoma. Nadhani utakubaliana na Mimi kwamba Adui mkubwa anayehatarisha Amani ya Taifa letu ni mfumo mbaya wa chaguzi zetu na ubovu wa katiba yetu.
Umekuta watu wanapambana na huyu Adui kwa manufaa ya Taifa, unawaambia sawa pambaneni naye tuko pamoja. halafu wewe unaanza kuwabeza kwa namna wanavyopambana na Adui. Hii haijakaa sawa.
Kwa kuwa wote tunakubaliana Adui yetu ni mmoja basi hatunabudi kuungana, kupigana kwa pamoja kila mtu na silaha yake kuhakikisha Adui (anakufa) anaondoka Nchini kwetu.
Kama unavyojua vita, hapa kutakuwa na upotevu mkubwa wa Maisha, mali, Maslahi na hata wengine kupata ulemavu wa kudumu. Hapa ndipo ninapouona ugumu wa Watanzania wengi kupambana na Adui yetu huyu.
Tupambane kwa kesho ya Taiga letu.
 
Mkuu Cute Wife ,ubarikiwe sana kwa elimu hii!,mimi nimepandisha humu mabandiko zaidi ya 100 kuomba mabadoliko ya katiba,kurejesha haki ndani ya katiba yetu!。

Kwa vile,tumeomba sana,kupitia maandiko, sauti, vipindi vya redio na TV, she did nothing!,before the last final,attempt,nafanya utafiti if she is innocent genuine,kama ni kweli hajui,tutamsamehe,
Inawezekana ni Kiburi na Jeuri or Real Busy? Wasaidizi wake hawajamwambia ukweli wa ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?,Tufanye nini kupata Haki? lakini kama ukweli anajua ila ni anatufanyia kiburi tuu na jeuri ya madaraka na mamlaka, then。。。!

P
Pokea maua yako Mkuu.
 
Chawa chawa:BearLaugh::KEKLaugh: yaani siku hizi ni mwendo wa kububujikwa machozi ya huzuni tu... kila mnapogeuka mnalabuliwa... lazima mkae mguu sawa saivi:KEKWlaugh::KEKWlaugh::pepeLaughers:
My lady,
chukua hayo mambo matatu ni muhimu sana kuyazingatia kuelekea uchaguzi mkuu wa October mwaka huu 2025, ukamueleze na mwenyekiti wa chama chako na itapendeza sana,

huna haja ya kubabaika sana 🐒
 
Mkuu Bra, Bra-joe ,kwanza asante kwa objectivity yako kwasababu hii jf ya kisasa,kupata watu objective ni wakutafuta kwa tochi!

Ni kweli kabisa,Lissu, Chadema na wapinzani, wana hoja ya msingi kabisa kuhusu ubovu wa katiba yetu na udhaifu wa chaguzi zetu, hivyo hitaji la reforms,ni hitaji la msingi sana!。

japo madai ya upinzani ni madai ya msingi,the approach ya kudai is a wrong approach,huwezi kusema no election!,rais mwenyewe wa nchi hawezi kusema no election!,who are you useme no election?!。

hapo kuna matatizo both ways,media isiyotenda haki kwa wapinzani,na wapinzani wasiojitambua na kufanya siasa za hadaa,utopian politics。

hapana,

huu ni mtazamo wake。
P
Sasa rais atasemaje no election wkt yy ndio mnufaika wa election yenyewe pascally mbona unazeeka vibaya hivyo
 
Wakuu,

Mwaka 2022 Mahakama ilibatilisha kifungu cha 11 (1) (c) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kinachoweka zuio kwa wafungwa wanaotumikia adhabu ya kunyongwa na wanaotumikia adhabu ya kifungo cha zaidi ya miezi 6 kujiandikisha ili kupiga kura.

Hivyo kwa kufuta kifungu hiki ilifanya wafungwa wote wa makosa ya kawaida ya jinai kuwa na haki ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu bila kujali muda ambao wametumikia gerezani.

Hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Elinaza Luvanda inatokana na shauri la Kikatiba lililofunguliwa na raia wawili; Tito Magoti na John Tulla ambao walikosa haki ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kutokana na kuwa mahabusu (japokua Sheria ilikua inakataza wafungwa na sio mahabusu) ambapo walidai kuwa kifungu hicho kinakinzana na Katiba Ibara ya 5(1) ambayo inaeleza kuwa kila raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 anayo haki ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu.

Sheria mpya ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024 imeendelea kuwa na kifungu hiki kilichobatilishwa na Mahakama kwa kuendelea kuwanyima haki wafungwa kushiriki katika uchaguzi kwa kuwa hawana vigezo vya kujiandikisha kupiga, ambapo Kifungu cha 10(1)(c) kimesema wafungwa waliokuhumiwa kifo au kifungo zaidi ya miezi 6 hawatakuwa na haki ya kupiga kura!

Hivyo basically hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika kwasababu hata mwanzo wanaotumikia kifungo cha chini ya miezi 6 walikuwa bado na haki ya kupiga kura. Serikali imeendelea kukaidi amri ya mahakama iliyobatilisha kifungu kinachomzuia mfungwa kupiga kura (wakati Haki hiyo imetolewa kikatiba) na kukirejesha katika Sheria mpya ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani chini ya Kifungu cha 10(1)(c) kinachozuia wafungwa kujiandikisha na kupiga kura.

Pia soma: Makalla: Wafungwa chini ya miezi sita (6) watapiga kura Uchaguzi Mkuu

Hata Kifungu cha 42 ambacho anasema kinamruhusu kila mtu kupiga kura

kimewekewa kizingiti/kigezo kwamba lazima mtu awe amejiandikisha, lakini huwezi kujiandikisha kama hujakidhi vigezo, na kigezo kimojawapo ni kwamba hutakiwi kuwa mfungwa wa adhabu ya kifo au mfungwa wa zaidi ya miezi sita, sasa hii inamaanisha hamna mabadiliko yoyote makubwa yaliyofanywa au hata madogo kuhusu ushiriki wa wafungwa kwenye uchaguzi wa Urais kama anavyotupanga.

Team chawa ukiongozwa na mama anatosha Lucas Mwashambwa ChoiceVariable Tlaatlaah johnthebaptist mbebe na wenzenu mjeeee:BearLaugh::BearLaugh: msisahau kumbeba mwanasheria Pascal Mayalla awasaidie kusoma maandishi kwa uzuri
Makalla mzee wa hovyo sana CPA chawa
 
Kw
Ni inaonekana ni kama,sijawahi kuegemea upande wa serikali。

kwa mujibu wa fani yetu,sisi。media ni non partisan, tunapaswa kuwa neutral wakati wote.

media tukaa upande wa wakweli,kama wakandamizaji ni wa kweli,tunasimama nao!。

Nimekusikia。
P
Kuwa mkweli, kwenye mkutano wa media na TAL, uneutral wako uliuweka mfukoni na ukaonesha sura yako halisi kwamba upo upande gani!

Maswali yako yote uliyojenga kumuuliza TAL, tayari yalikuwa yashajadiliwa sana humu JF na kupatiwa majibu kwa ufasaha kabisa kwamba Ssh kwenda Nairobi kumuona majeruhi haikuwa safari iliyopangwa, bali alipitia kwa kujibaraguza, kujikosha na 'kuzuga'.

Halafu la kumwachia Mbowe haikuwa hisani bali ni takwa la kisheria kwa sababu ilikuwa ni kesi ya 'kubumba', yote hayo wanaJf tulikuwa tushayafanyia kazi.

Kuibua maswali ya namna hiyo ambayo majibu yake halisi ulikuwa nayo, kwanza hadhira ilikuona kuwa wewe ni chawa na muumini wa mi5 tena kindaki ndaki.

Wanyumbani uliboa na ulituchosha sana mashabiki zako ujue!
 
Back
Top Bottom