Sijui ni mimi tu au ndio watu wameanza kunogewa na mahusiano ya mapenzi ambayo tunaweza kuyaita si ya kawaida. Nimefuatilia threads nyingi kwa wiki kadhaa sasa na nimekuta zenye kuvutia sana ni ziile ambazo zina dalili ya mahusiano yasiyo ya kawaida. Yaani, watu wanakuja na stori mbalimbali za mahusiano ambayo yanakaribia kuvuka mpaka wa weird na kuwa sexual perversion.
Mara mtu kamtamani baba mkwe
Mara mama mkwe anakula chabo
Mara fulani kalala na dada wawili
Mara Kijana kalala na dada yake
Mara kaka kaota anachakachuana na dada zake
Mara baba kamnunulia chupi binti yake
n.k
Ninajiuliza hizi ni fantasy tu za incest au ni kweli sasa tumeanza kuvuka mpaka wa mahusiano ya kawaida kiasi kwamba ukiwaona dada na kaka wanatembea na kuchekeana unaanza kuhisa wanaumana na kutafunana; ukikuta baba anamkumbatia binti yake kwa ku-hug unafikiria labda usiku anachombezwa! Yawezekana kuna tatizo mahali fulani ambapo watu wanaanza kupoteza mipaka ya miiko ya kingono (sexual morality) na sasa imekuwa kile mtu anatamani au ni njozi tu za mapenzi watu wanaanza kukifanyia kweli. yaani, tunaanza kuvunja vunja mipaka yote ya kimapenzi na kile "mundu ave na vake"! hata kama huyo "wake" ni mtu wa miiko.
Labda ninachouliza kwa maneno machache, je miiko ya mapenzi ipo tena au ndio kula kulaana?
Vinginevyo itabidi tuwaombe ma MoDs waanzishe aidha mada ya watu wa mahusiano ya kawaida au watu wenye njozi za ajabu ajabu wajifungie humo ndani. I'm just saying. Wengine bado na uzee tunataka mambo ya boy meet girl, girl meet boy, boy's heart broken, girl cry.. just the old fashioned romance and love stories. And of course the old visa vya uswahilini!