Hakuna mahusiano ya "kawaida" tena?


Japokuwa kuna umuhimu wa kuwa na a proper system ya kuelewesha vijana wetu ili waweze kutofautisha mabaya na mazuri.The whole society is so messed up,kama sie wakubwa tunakuwa confused hivi,sijui tutawaficha wapi watoto wetu!
 
MMK; ndiyo maana nakumbuka enzi zile ya the bold and the beautiful, mama yangu alikua ananiambia kwanini naangalia takataka ambayo haina mafunzo mazuru katika maisha zaidi ya kukufundusha "mwanaume ana lala na mama, alafu na mtoto etc..." Siku hizi TV ina mambo mengi ambayo nitofauti na yale ya zamani.. na hamna control juu ya vitu watoto au vijana wana angalia siku hizi...

Wao wana kwambia wana enda na wakati... Wewe unaishia kufikiri wakati unaenda bila wewe..
 
MBU uko wapi??

...nipo dada'ngu wee!

Unajua, pale juu kuna kipengele kinasema JF Where We Dare Talk Openly, ...Jamii Forum iwape nini tena!
Miaka ile ya nyuma, 2007, 2008, 2009 na kidogo mwanzoni mwa 2010 kulikuwa na mada zenye
kuchangamsha vichwa, ambazo zilivutia wengi kulivamia na kuchangia jukwaa hili.

Bahati mbaya, au nzuri...umri unakwenda, vijana wa 80's wanabaleghe nao. Kwa kujidhania wapo 'huru' nyuma ya mtandao na Pen names (Anonymous) wanazotumia, wengi wao wameamua kuufanya ukumbi ni kikao cha karata na kupiga soga.
These days nakutana na topics zinazonistaajabisha IQ za muanzishaji na wachangiaji, mfano;

  • Hivi kuna Mwanaume hajawahi kupiga Punyeto?
  • kwanini mademu wanasikia kiu
  • Nikiwa kifuani
  • Nilianza mwaka kwa kufumaniwa.
  • Mume Kuvaa Kanga - Wakati Gani Unafaa?
  • nk...
Mada hizi hupata wachangiaji wengi kwani haziwaumizi sana akili kutafakari kabla ya kujibu.
Mzaha mzaha hutawala kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Jambo la msingi, maveteran na wale wachangiaji mahiri waendelee kuleta mada za maana, na kuacha kuchangia topics zisokichwa wala miguu
...otherwise, jamvi la MMU linaelekea kugeuzwa 'Darhotwire.'
 
Nahisi ni watu wanatafuta popularity na idadi kubwa ya visitors at any cost. Jamii yetu ya kitanzania kwa uhumla inapenda sana kushadadia mambo ya ajabu. Angalia mafulliko ya magazeti ya udaku na habari zao!!!!!!!!!!!!
Big up uliye leta hili swala jamvini na kama tunajali na kuupenda utu wetu lazima tuyakemee haya kila maaala.
Kuna vitu vibaya unapo publicize ndo unavijenga zaidi. MoDs please take care of this.
Pia nashauri uwe msukumo mkubwa zaidi kwa vyombo vya habari za udaku pia viwe regulated.

Good Night membres..
 
najua kuna baadhi ya mambo,sio mazuri kujadiliwa,lakini hayo mambo yapo,na kuna baadhi ya watu,wanaona njia rahisi ni kuyaweka humu,kwani hakuna anaemuona mwenzie.kwa upande wangu,mambo mengi yamenishangaza humu,na mengine nimejifunza humu,ambapo nisingeweza kumuuliza ndugu yangu au rafiki yangu.mimi naamini kila binaadamu ana muonekano wake wa maisha,na maisha jinsi aliyokulia na malezi aliyolelewa
 
ICHUKULIE KAMA NI SEHEMU YA KUJIONGEZEA MAARIF NA KUJUA DUNIA INAKOELEKEA.... NADHANI UNA PRINCIPLES ZAKO ZA KIMAHUSIANO... STICK TO THEM!!:love:
 
ICHUKULIE KAMA NI SEHEMU YA KUJIONGEZEA MAARIF NA KUJUA DUNIA INAKOELEKEA.... NADHANI UNA PRINCIPLES ZAKO ZA KIMAHUSIANO... STICK TO THEM!!:love:...UKIJARIBU KUFANYIA ZOEZI UWALUWALU WA HUMU MMU..... UTAJUTA NAFSIYO..
 
Kuna wakati mtu unatamani hizi threds zigeuke email kwenye inbox yangu, ili nizisweke kwenye trashbin...
Kiujumla baadhi ya wadau wa jukwaa la MMU wanlina-over rate suala la ngono...
 
Kuna wakati mtu unatamani hizi threds zigeuke email kwenye inbox yangu, ili nizisweke kwenye trashbin...
Kiujumla baadhi ya wadau wa jukwaa la MMU wanlina-over rate suala la ngono...

...nakuunga mkono 99.9%. Kwa wanaofanya research kwanini mahusiano ya mapenzi na urafiki yanayumba kwa kizazi hiki, anaweza kuandika thesis ya kujitosheleza kabisa kulingana na seriousness na upeo wa mawazo wa wachangiaji wengi.

Imefikia kwamba, hata wale walio na hoja za nguvu, wana opt kusaidiana mawazo kwa PM badala ya kutafuta ushauri wa jumla na kuishia kujiudhi na 'cheap replies!'
Anyway, it's JF Where We Dare To Talk Openly!
 
maisha bila miiko sio maisha ni laana...............
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…