Its Pancho
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 15,966
- 26,404
Wakuu
Huwa sipendi kuficha
Kwenye ndoa zetu hizi mama mkwe kumpenda mkwewe asilimia mia ni kitu ambacho hakiwezekani. Huwa wanawapenda ki-uongo tu na ki-nje nje. Sababu kubwa ni kuwa kutokana na upendo wa mama kwa mwanae huona Kama mtoto wake anapoenda kuoa inamaana yeye (mama) ni kama anamkabidhi mwanae akatunzwe sasa na mwanamke mwengine..! Japo haiwezekani mama kuzuia hilo lazima protocol ziende kama zilivyo. Matokeo yake
Mama kama anakaa hapo kwa mwanae Visa vitaanza dhidi ya mkwewe kila kukicha visivyo na kichwa wala miguu. Na sisi watoto wa kiume tunajikuta tunamsikiliza mama zaidi kwenye utetezi wao wote wawili.
Kumbe tunawaumiza wake zetu sana na huenda wanatupenda sana na ndo maana wameamua kuishi na sisi majumbani na kuondoka kwao,
Kuchukua jina lako na kuacha la baba yake.
Nakumbuka nilipokuwa mdogo mama yangu aliteseka sana kutokana na usumbufu na ugomvi usiokwisha kila siku kutoka kwa bibi mzaa baba (alikuwa katoka musoma) .
Siku nyingine akisalimiwa haitiki usiposalimia anasema kwa baba kwamba mkewe (mama) ni jeuri.
Siku moja mama alikuwa anamwaga maji nje na bibi amekaa mbali kwenye mkeka ghafla akaanza kupiga kelele(bibi) huku akimuita baba
"mwenga amenimwagieko maji "
Kwamba mama amemwagia maji mguuni. Huku analia. Akaulizwa yako wapi uliyomwagiwa? Hakuna..! Kakazana tu anasema atamlaani baba kisha anatishia kubeba mizigo arudi musoma...! Visa vingine vingi.
Since kipindi hicho nimejifunza mke ukae nae wewe na mama yako asikae hapo mjengee nyumba jitahidi au kama ana kwake na baba waache wakae Wale uzee wao..
Usijaribu