Mi nadhan sisi wadada tunaoolewa ndo tuna matatizo kuweka negative perspective kwa wamama wa waume zetu/mawifi/mashemeji na hii nadhan inatokana na kukaririshwa na jamii inayotuzunguka kiasi unakuta mtu anajiandaa kabisa kutoa negative reaction kwa huo upande lengwa...tunawapa wakat mgumu sana waume zetu kutengeneza balance ya upendo na wengi wao maamuzi yao ni kuhama kukaa mbali na wazazi wao.. lakini wengi wetu hatujawahi na hatujiulizi sisi hatuna wazazi?? Hawatukwazi??
Hawatuendeshi?? tulishawahi kutaka kuwakimbia??.. kama uliweza Kum tolerate mzazi wako why not mzazi wa mwenzio mnaeshare nae kitanda kimoja kwa shida na raha!!tujue kabisa huyo unaemuona mume wako ni mtoto wa mwenzako umekutana nae akiwa na meno 32,amelelewa kuna wamama wengine wamesacrifice a half of their youth age ili kutengeneza huyo responsible man unaemwita mume wangu kwa shida na tabu..
Bas usimbane 24/7 hebu mpe muda wa Ku spend na mama ake bila ya wewe kuwepo, bi mkubwa ajielezee wee mpaka hamu imuishee.. af uone kama kutakuwa na troubles... Shida ni moja tu wakaka mkishaoa hamna mda wa kukaa na mama zenu wawadekee na kuwaeleza shida zao private mda wote ukitoka kazin umekula zaidi ya shkamoo mama upo ndan na mkeo kwanini wazazi wenu wasiseme wamemwagiwa maji ya moto ili angalau kupata ile attention yenu.. hiv hamjui mtoto wa kiume akishakuwa mkubwa anakuwa like a second husband to his mum hebu wakaka zetu mjitahidi angalau kwa wiki mara moja mjitengee ka muda ka kukaa private na mama zenu ati ha ha haaaa