Siyo kweli!
Mbunge anapaswa kuwa na Dira ya Maendeleo ya watu wake kwa kuweka vipaumbele vya Jimbo lake vizuri!
Siyo kila kitu kinafanywa na Serikali!
Watu wakijiongoza vizuri na kuweka malengo ya pamoja kama watu wenye nia ya kwenda kwenye hatua fulani walioichagua basi Wanajimbo wanaweza kufaulu kusogea mbele kimaendeleo.
Chukulia Mfano tu wa Jimbo ambalo Maendeleo yake huletwa na Kilimo.
Halafu Mbunge wao hana Shamba na akiwa nalo basi liko hoi...huyo hafai kuwa Muwakilishi wa watu wake kwa Sababu alipaswa kuwa na Shamba la Mfano kwa ajili ya kunyanyua wananchi wenzake.
Mbunge ana influence sana kwenye Jimbo lake hata kama Serikali haina pesa!
Hata kwa tabia ya Usafi wa Mazingira tu; hilo halihitaji Pesa ya Serikali lakini linahitaji kuwa na Kiongozi mwenye Dira...!