Hakuna 'mchepukaji' mwenye sanaa ya upendo

Hakuna 'mchepukaji' mwenye sanaa ya upendo

Matteo Vargas

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2019
Posts
803
Reaction score
1,329
Kwanza tujue upendo ni nini kwa mujibu ya Biblia Takatifu.

Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli. (1 Wakoritho 13: 4-6)

Kabla sijaenda mbali tafakari hayo maneno ya Biblia hapo juu kwenye ndoa au mahusiano yako yanafanya kazi kwa asilimia ngapi?

Back to the topic:
Siku hizi upendo kwenye mapenzi umekuwa ni wimbo uliokosa muimbaji. Watu wanasema wana wake, wana wapenzi lakini hawana mapenzi. Uongo na uchepukaji vimekuwa vitu vya kawaida leo hii kitu kinachopelekea baadhi wa watu kukosa ladha halisi ya mapenzi badala yake wanabaki na vidonda vya mapenzi.

Unaweza ukawa unasoma huu uzi muda huu lakini mpenzi wako yupo na mtu mwingine anaemuita mpenzi pia (ushishtuke relax), sasa kati ya wewe na huyo aliye nae muda huu wote mnaongopewa kuna mwingine anaempenda zaidi yako na huyo ambaye yupo nae sasa huko lodge au gheto. (Acha nishushie Alkhasusi hata mimi wa kwangu sijui kinachoendelea 😔)

Ukweli mchungu ni kwamba wengi wetu tuli-enjoy sana mapenzi kipindi tupo shule hasa hasa miaka ya 2000 hadi 2010 wakati tupo O'level au A'level kipindi hicho ilikuwa ukitumiwa barua au picha siku hiyo hata njaa husikii😆 ila bahati mbaya zaidi wapenzi wetu hao sio tulionao kwa sasa. Unamkumbuka mpenzi wako wa kwanza kabisa ambaye ilikuwa ukimuwaza tu ulikuwa unajisikia furaha. Uliyenae sasa ukimuwaza unafurahi na kutabaamu au tusifuatilie maisha yako?😆😆

Tunaposema sanaa ya upendo ni kitendo cha mpenzi wako kukujali na kufanya uwe na furaha muda wote bila kujali mtu huyo ana kitu au kitu. Umewahi kujiuliza kwanini kipindi tunasoma tulikuwa hatuna hela wala magari lakini tulifurahia sana mapenzi? lakini leo watu wana kila kitu ila wanafika muda wanachokana? Hakuna sanaa ya upendo.

Siku hizi mtu kuchepuka imekuwa life style, mtu kuwa kwenye mahusiano na watu 4+ ni jambo la kawaida, sasa hiyo nguvu uliyowekeza kwa watu 4 ungeiweka kwa mtu mmoja huwezi kufurahia mapenzi? Unapokuwa na mwanaume au mwanamke zaidi ya mmoja huwezi kuwa mbunifu kwenye mapenzi unajawa na hofu ya wizi sio wewe wala huyo unaye-mcheat atafurahia mapenzi kwa namna yeyote Ile sababu hakuna mchepukaji anayeweza kuwa na sanaa ya upendo sababu anaongozwa na tamaa ya ngono au vitu.

Hakuna mchepukaji mwenye sanaa ya upendo wote ni matepeli.
 
Back
Top Bottom