MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
Kiufundi nawaogopa zaidi Azam FC kuliko hata Yanga SC kwani Azam FC wana Wachezaji wenye Vipaji Asilia huku Yanga SC wakiwa na Wachezaji wenye Ushindani na Morali ya Juu.
Hakuna Mechi ambayo inaniumiza Kichwa Kuiwazia mpaka kuwa na Hofu nayo kama hii ya leo kati ya Simba SC yangu dhidi ya Azam FC na kinachoniumiza Kichwa zaidi ni kuona Watani zetu Yanga SC nao ndiyo Kwanza wakizidi tu Kuchanja Mbuga kwa Ushindi huku Kiwango chao kila Siku kikizidi tu Kuimarika na kuonyesha kuwa kweli Msimu huu wamepania na wana Jambo lao.
Kama kuna Mtu ambaye atakuwa na Furaha Kubwa leo Simba SC ikishinda dhidi ya Azam FC basi ni Mimi kwani naiona hii Mechi ni ngumu, imekaa vibaya Kwetu na Azam FC watakuwa wamejiandaa nayo Kiufundi na Kimkakati pia.
Sijui kwanini kuna Hisia zinaniambia kuwa kama Simba SC tutashinda leo dhidi ya Azam FC basi ni kwa taabu mno ila kuna Uwezekano pia ama Simba SC tukatoka Sare au Suluhu na tunaweza vile vile tukafungwa na Kuuanza mwaka 2022 vibaya. Wale waombaji basi leo tuiombee sana hii Mechi ili tushinde kwani nina wasiwasi nayo mno.
Mungu ibariki tu Simba SC yangu leo!!!