Mkuu waganga wapo wa uhakika kabisa,
Yaani mkono kwa mkono,
Siku 3 unapata majibu.
Tatizo kuwapata ni ngumu sna,
Ila wapo na ushuhuda upo.
1
Kuna dada mmoja alikuwa mteja wangu sana. Yeye alikuwa na mgahawa. Sasa akaanza kusikia kama vichomi begani, bega la mkono wa kulia. Siku 3 za mwanzo toka apate hilo tatizo alikuwa akija kununua mazaga yake analalamika "Kizibo, mimi naumwa, naumia begani.
Hapo ilikuwa mwezi 8 mwaka huu. Ebwanae, mkono ukawa mkono, ukaanza kuuma ile kisawa sawa na ukaanza kujaa (kuvimba).
Akaanza kwenda hospitali. Pima sana hakuna kitu. Akapewa madawa ya kuchua na vidonge vya kumeza..wapi!!
Akabidilishiwa tiba, ikabidi aanze kuchoma sindano..wapi!!!!
Ikabidi aangalie upande wa pili. Hapo bado anaweza kutembea na kuongea vizuri tu. Akapata mganga, akanishirikisha nikampa Tsh 20k. Akaenda akakaa huko siku 3, bila bila, maumivu yanazidi kuwa makali na mkono unazidi kujaa. Muda huo wa siku 3 alipokuwa kwa mganga sikuwa nawasiliana nae.
Siku kama ya 4 toka aende kwa mganga, siku hiyo Mida ya saa 11 jioni akanipigia simu, kupokea tu maneno aliyoniambia yalinivunja moyo. Kwa sauti ya kuchoka na ya uonyonge...
"Hallo, Kizibo rafiki yangu upo wapi? Njoo unione nakufa".
Nilipofika tu na kumuona almanusura niangue kilio. Binti kakonda, kawa mweusi halafu mkono umevimba sana na umeota maupele yanayotoa maji maji.
Nilipofika akasema..
"Kizibo umefika? Mungu akubariki sana. Kama unavyoona, hali yangu ndio hii, kwa hapa nilipofikia siwezi kuendelea, siwezi"
Daah, ikabidi nitoke nje nikaongee na mama yake, aliyekuwa nje yupo kama amepagawa asijue la kufanya. Mama akaniambia kuna mtu inasemekana ana uwezo wa kutibu huu ugonjwa, "tumeambiwa na baba mmoja ambaye binti yake alitibiwa na huyo mama, ndo tunamsubiri aje".
Nikasema wafanye haraka aje aanze kumtibu na kuhusu gharama za matibabu iwe juu yangu
Jioni huyo mama alifika na kuanza kumtibu, alikuja na dawa fulani ya kumpaka ikiwa imechanganywa na mafuta. Kuanzia jioni hiyo, huyo dada alianza kupata ahueni, na baada kama ya siku 4 hivi binti alikaa sawa. Malipo ikawa elfu 30, nikampa akamlipa yule mama.
Huyo mama aliemtibu sikuwahi kumjua, kumuona wala kuwa na mawasiliano naye. Ila naweza kuipata namba zake ikiwa 100% compulsory needed.
Baada ya kupona, yule binti nilimla mara 1, na kabla ya kuugua nilikuwa nishamla mara 1. Yeye na mama yake wakataka eti nimuoe, nikawakwepa. Binti akamaind, akarudi kwao kijijini na namba zake hazipatikani hadi sasa.
N.B: Huyo mama nadhani sio mganga. Ni wale wamama unakuta anajua dawa fulani halafu ametulia tu, mtu akiwa na shida akielekezwa kwake ndio anaenda anamtibu.
2
Mwaka 2021 nadhani, tarehe kama 20 au 21 December, niliumia mguu, kwenye ankle. Ilikuwa usiku wa saa 2 hivi, ndani ya dakika 10 mguu ushaanza kujaa (kuvimba). Kesho asubuhi nilikuwa niwezi kuukanyagia hata kidogo, kwanza usiku sikutaka, ulikuwa unauma balaa.
Sasa kuna mama jirani yake na kaka, bro akaniambia njoo mama fulani akuangalie. Nikafika pale kwa bro mida ya saa 2 asubuhi, nilipelekwa kwa piki piki huku nina gongo la mti. Kwa kuwa yule mama alipewa taarifa usiku hakutoka. Akaitwa akaja. Alikuja na majani fulani ameyaponda ponda, akayachanganya na mafuta mgando. Akanikanda hiyo saa 2. Nusu saa baadae nikaanza kuwa naukanyagia ule mguu. Akanikanda mchana. Aah saa 10 nikaenda na kutembea kwa majirani huku nachechemea.
Akanikanda usiku, na kesho tena asubuhi. Mchana wa siku hiyo hiyo ya pili nikamwambia aniandalie dawa ya kwenda nayo niwe najikanda huko huko kwangu. Siku hiyo nikarudi mzigoni (kazini) kama kawaida.
Kwa jinsi nilivyokuwa nimeumia kwa kawaida ningekaa ndani si chini ya wiki 2. Nasema hivyo kwa sababu nahisi kuna kamfupa kalipata crack au fracture kwa mbali maana hadi sasa ninapasikia kwa mbaali halafu kama kuna kanundu fulani hivi