Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Mbeya inawezekana ndio jiji lenye miondombinu mibovu zaidi na makazi yasipangaliwa na duni pia, kuna nyumba za udongo na vijumba vya ajabu ajabu katika jiji!
 
Walitumia vigezo gani kuupa mji wa Mbeya kuwa jiji mbona kama pako local sana hata baadhi ya miji hapa Tanzania ambayo sio majiji inaizidi [emoji848]
Itakuwa siasa tu
 
Maranatha Hospital U/C in Mbeya.

Hii itakuwa Hospital kubwa sana
 
Mbeya inawezekana ndio jiji lenye miondombinu mibovu zaidi na makazi yasipangaliwa na duni pia, kuna nyumba za udongo na vijumba vya ajabu ajabu katika jiji!
Mji gani uliopangwa Tzn hii?

Arusha,Dodoma na Mwanza sio tuu Kuna nyumba za tope Bali ni kama mabanda ya nguruwe
 
Mhhh ila Kwa hii mbeya hapana, kipindi Cha kiangazi Kuna vumbi sana, nyumba nyingi Zina quality Duni, huwezi amini hadi kipindi hiki Cha mvua huduma ya maji ni ngumu kupatikana Kwa maeneo mengi hapa mbeya. In short naishi tu mbeya ila nikipata fursa ya kuhama ni haraka sana nafanya hivyo
 
Kizuri cha kwao wenyeji wa huko! Ila mimi kusema kweli Mbeya uzuri ni chakula tu!
Ila mji wao ni mbovu na hauna mvuto wowote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…