Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Sana. Nawaza tutawasaidiaje hawa watu vilaza namna hii.Tatizo la Afya ya akili linaendelea kuwa shida Kwa watu wengi sana 😁😁
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sana. Nawaza tutawasaidiaje hawa watu vilaza namna hii.Tatizo la Afya ya akili linaendelea kuwa shida Kwa watu wengi sana 😁😁
Hayo ndio ya Maskini Sasa Mwanza unaijua? Maskini na matajiri wamechanganyikana humo humo,hakuna mitaa Kila sehemu ni uswazi na Kuna nuka 😁😁Mbeya hakuna mji pale hasa mjini imekaa kama kijiji.
Maeneo yafuatayo ni mbeya mjini chini ya kilometer 2 kutoka city center lakini yote ni hovyo kwa mtogole tandale irudi shule.
Sinde
Ilolo
Mabatini
Isanga
Iwambi
Ilemi
Itende
Ilomba
Hovyo kabisa
Kidogo forest ndio kidogo sana waweza sema mji
Shida ya Songea ni rangi nyekundu ya vumbi 😁😁Nimeishi mkoa wa Mbeya miaka 3 ni best place ever in TZ ,Bila kusahau kwa watani zangu Songea ni pazuri sana nyanda za juu kusini kuna uzuri usio na shaka
mbeya moja
soko matola moja hiyo
Ngoja wachangiaji wengine waje tuskie wanase.a nini kuhusu mbeyaMkoa wa Mbeya ni Kati ya Mikoa mitano iliyopo Nyanda za Juu Kusini sanjali na Mikoa ya Ruvuma, Iringa, Songwe, Njombe na Rukwa. Mbeya ilianzishwa mwaka 1961.
Mkoa wa Mbeya umejaaliwa kila kitu unachokijua wewe.
Kwa hapa Tanzania sijaona Mkoa Mzuri wa Kuishi kushinda Mbeya.
1. Kiuchumi
Mbeya ni ya 3 Kwa kuchangia pato la Taifa yaani GDP Tanzania.
Mbeya ni ya 3 Kwa kuwa na Watu wenye kipato kikubwa.
2. Hali ya Hewa na Mandhari
Mbeya Ina Hali ya hewa ya majira yote yaani Bariadi na joto na mvua ni uhakika sio tia maji tia maji kama Mikoa mingine.
3. Usafiri
Uwanja wa ndege wa Songwe
Usafiri wa Barabara kutoka Mikoa yote na Nchi jirani Kupitia Barabara kuu ya Tanzam. Usafiri wa kwenye Maji via Ziwa Nyasa. Pia Kuna usafiri wa reli nzuri kabisa unakufikisha Zambia kutokea Dar.
4. Kilimo
Mbeya Ina Ardhi nzuri ya kulima Kila aina ya zao kuanzia mbogamboga, matunda, nafaka Hadi pareto na chai.
5. Madini na Nishati
Mkoa una Kila aina ya Madini kuanzia Dhahabu za Chunya Hadi Makaa ya Mawe ya Kiwira bila kusahau Madini ya gas asilia ya CO2. Umeme ni wa uhakika unaozalishwa kutoka migodi ya Kiwira na Geothermal.
6. Elimu
Mbeya ni Kati ya Mikoa ya Wasomi hapa Tanzania. Mkoa wa Mbeya una vyuo Vikuu zaidi ya 5 mfano MUST, Mzumbe, CuCoM, UDSM, Tumaini, nk.
Mkoa una mamia ya vyuo vya kati na shule za kutosha eg St.Francis hivyo ni ideal pia Kwa issues za Elimu.
7. Utalii
Hapa kwenye Utalii ndio Kuna fursa nyingi maana sehemu kubwa ni underdeveloped.
Kuna Milima ya Kawetere, bwawa la Mungu, Hifadhi ya Kitulo na pia unafika Kwa urahisi Ruaha au Katavi NP kutokea Mbeya.
8. Viwanda na Biashara
Kuna viwanda vya aina mbalimbali kama Saruji, vinywaji vikali na laini kama soda, bia, wine nk.
Kuna viwanda vya magodoro, vifaa vya ujenzi, home appliances nk.
Aisha kama unataka kujenga viwanda Kuna maeneo ya kutosha yametengwa Kwa Ajili hiyo.
Mbeya ndio Kitovu Cha Uchumi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
9. Makazi na Accomodations
Kuna fursa kubwa Bado ya ujenzi wa hoteli za kitalii na hoteli za kawaida maana ni Mkoa wa Biashara hivyo itakulipa.
Pia Hapa ni wewe tuu maana ujenzi wa Mbeya sio costful kama Mikoa mingine,unachagua ijengee tofauti au blocks au hata tofari mbichi udongo una nata vizuri kabisa.
10. Watu
Mbeya Ina idadi ya watu zaidi ya milioni 2.3 Kwa Mkoa mzima wanaokuhakikishia soko.
Aidha watu wake ni Wapambanaji ndio maana huwezi kusikia Mbeya ikitajwa kwenye mambo ya umaskini na shida ndogo ndogo,hawalalamiki kusubiria serikali.
11. Michezo na Burudani.
Mbeya Ina Wasanii wakubwa Toka kitambo ila icon ya Mkoa ni kina Sugu,VanBoy na Stamina.
Kwenye Michezo hapo ndio nyumbani hususani football.Mbega Ina Timu 3 Ligi kuu za Prisons,Ihefu,Mbeya City na Timu 3 Ligi daraja la kwanza za KenGold,Mbeya Kwanza na Tukuyu Stars.Na Ina Wachezaji Wakubwa wengi tuu na makocha.
Kiufupi hiyo ni summary ndogo sana Kati ya Mengi mazuri yaliyopo Mbeya,Karibuni sana Mbeya.
Haijalishi wanasemaje ila Mbeya ni tamu sanaNgoja wachangiaji wengine waje tuskie wanase.a nini kuhusu mbeya
Hujakosea bwasheeMbeya ni mkoa aisee