Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Ukiacha la Ukimwi, mengine chumvi imezidi na Kila Mji yapo zaidi ya hayo.
 
Mleta uzi hivi mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira umewahi kufika kweli? mgodi umechoka hauzalishi umeme,nimewahi kwenda usiku hadi nikasikitika,kwa sasa wanatumia umeme wa TANESCO,unaotoka Kidatu
Umefufuliwa na unapiga kazi.

Pili Kwa taarifa Yako tuu Kiwira haiko Mbeya Iko Mkoa wa Songwe Wilaya ya Ileje
 
Nakubali Mbeya haikutokea kuwa hivyo by chance. Nchi ime-invest hela nyingi kwa ajili ya infrastructures, masoko, elimu na yote uliyosema kwa sababu ni mkoa mkubwa kati mikubwa michache inayoilisha nchi yetu kwa chakula pamoja na mikoa mingine ya kusini. Mvua ni nyingi na ziko evenly distributed. Naongezea tu sifa za Mbeya. Kwa vigezo hivyo huwezi kulinganisha na maeneo kama Kigoma, Geita au Simiyu ingawa ni wajibu wetu kama kuiweka vizuri ipendeze kama Mbeya eti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…