EvilSpirit
JF-Expert Member
- Jun 15, 2017
- 13,579
- 21,407
Huu ndio mchakato wa kuomba mikopo ya halmashauri maarufu kama mikopo ya asilimia 10 huanzia ngazi ya kitongoji, kijiji au mtaa.
Katika hatua hii ya mwanzo, kikundi cha watu wasiopungua watano kinapaswa kuundwa kwa ajili ya kupatiwa mkopo, na lazima kitambuliwe rasmi katika ngazi ya chini. Ili kufanikisha hilo, mtendaji wa kijiji au kitongoji hutakiwa kusaini na kupiga muhuri barua ya maombi ya usajili wa kikundi. Hapa ndipo mara nyingi rushwa huanzia.
Barua hiyo hiyo hupelekwa kwa Afisa Maendeleo wa Kata ambaye naye hutakiwa kusaini. Huyu mara nyingi hubadilisha mchakato huo kuwa kama mradi wake binafsi, ambapo atakuambia kuwa usajili wa kikundi unahitaji Shilingi 150,000.
Wapo baadhi yao ambao ni walafi wa kupindukia; hata baada ya kupewa kiasi hicho cha fedha, huendelea kudai fedha zaidi wakati mchakato ukiendelea, kwa mfano kwa ajili ya kuwaandikia muhtasari wa mradi wa kikundi, au hata baada ya fedha kutoka atataka tena mgao mwingine.
Baadaye, barua ya usajili hupitia kwa Mtendaji wa Kata, ambaye pia anahitaji malipo kabla ya kuweka sahihi na muhuri wake. Kama kikundi hakijui namna ya kujisajili kwenye mfumo wa mtandao wa TAMISEMI, hulazimika kumtafuta mtu aliyekabidhiwa jukumu hilo ndani ya halmashauri husika. Huyu naye hulipwa, ingawa kazi yake inaweza kusemwa kuwa inastahili posho rasmi.
Baada ya kikundi kusajiliwa mtandaoni, taarifa hiyo hupelekwa kwa Afisa Maendeleo wa Kata (CDO), ambaye akiiridhia huifowadi kwa Afisa Maendeleo wa Wilaya (DCDO). Huyu naye huifikisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (DED), ambapo hatua zote zinahitaji kupitishwa rasmi ngazi kwa ngazi.
Afisa Maendeleo wa Wilaya ndiye anashikilia fedha hizo. Huwezi kuzipata bila kutoa kiasi fulani cha fedha kama "chai".
Kwa mfano, kama mkopo ulikuwa Shilingi milioni 10, kikundi kitaweza kupokea milioni 8 tu huku milioni 2 zikipotea kama "makato" ya siri. Isitoshe, kabla ya kupokea mkopo, kamati ya ukaguzi itafika kukagua eneo la mradi.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ni Mtendaji wa Kata, na ili ukaguliwe, lazima utoe fedha. Wakaguzi wakiridhika na mradi, ndipo wanapendekeza pesa zitolewe.
Baada ya fedha kuingia kwenye akaunti ya kikundi, mnapaswa kujaza mikataba maalum ambayo pia hupitishwa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji/Kijiji na Mtendaji, ambao nao huhitaji rushwa ili waidhinishe.
Inaonekana ni DED peke yake ambaye hafanyi vitendo hivyo vya kupiga fedha, lakini watendaji walioko chini yake ni walafi wa kiwango cha juu.
Ni muhimu pia kufahamu kwamba kama uko upande wa pili wa kisiasa (mpinzani), basi sahau kuhusu kupata mkopo huu. Zamani ilikuwa ni lazima uwe na kadi ya kijani ili upate mkopo huu.
MWISHO: Hakuna mkopo mgumu kuupata kama wa halmashauri.