Hakuna mkopo mzuri wa Serikali wa miaka 5

Hakuna mkopo mzuri wa Serikali wa miaka 5

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Nimesikitiswa sana na wale wasomi wanao jaribu kuaminisha Watanzania kwamba kuna mikopo ya bank za biashara mizuri kwa serikali. Mikopo yenyewe mingi ni ya miaka 5 na riba zinakuwa 8%~10%. Hii mikopo sio mizuri kwa serikali hasa ukizingatia uwezo wetu. Serikali kwa ushauri wangu

1. Wasikope chini ya miaka 10
2. Riba ya mkopo isizidi ukuaji wa uchumi mfano Tanzania ukuaji wa uchumi ni 5%~ 7% hivyo riba iwe hapo katikati . Kama mkopo ni kwa dollar isizidi 5% kwasababu mfumuko wa bei wetu unakuaga 2% zaidi ya USA

Mwigulu acha mikopo ya riba ya juu na muda mfupi hii inaongeza payment amount za mwezi na mwaka na kusababisha pesa nyingi kwenda kwenye mikopo.
 
Huwezi kunielewa huu ni ujumbe wa School mate wangu Mwigulu. Kama sio mtaalamu wa haya mambo huwezi kunielewa. Wewe endelea na topic nyingine za madongo na ushabiki hii sio size yako
You'll gonna see.
 
Kwa nini nchi tajiri kama Tanzania iendelee kukopa? ^Tar-tea-zo^ linaanzia hapo! Misappropriation na mislocation is public funds and resources. Hii ni ishara tosha kwamba nchi yetu (na Bara la Afrika kijumla) inakosa viongozi wenye njozi na uzalendo wa kweli.
 
Mkopo usijali muda. Vigezo viwe, Return on Investment, interest rate, tunaupeleka wapi?

Ukienda kwenye uzalishaji, kukuza uchumi, miundombinu ya uhakika kama umeme, kilimo, maji, barabara, SGR utasaidia wengi, baadaye kuongeza pato la Taifa hivyo deni kuweza kulipwa.

Sio kwenda kujenga matundu ya choo, madarasa Kwenye Corona campaign, Kuchanja watu. Huwezi kurudisha pesa kwa style hii.

Tozo, kodi zinatosha kujenga madarasa.
 
Mkopo usijali muda. Vigezo viwe, Return on Investment, interest rate, tunaupeleka wapi...
Hao watawala bubu hawaelewi ^key-two^ hapo! Calculations zao, wakope na kuzitumia immediately, but tozo na kodi zifuatie baadaye ziwe zinafagia mauchafua yao taratibu kwa muda mrefu hadi pasafike. Umeelewa sasa?
 
Halafu 21% inaenda Zenji. Uhuni mtupu.

UK wana muungano (England Scotland, Nothern Ireland, Wales) wanatumia kitu kinaitwa Bannett formula.

Kila nchi inapewa pesa, pesa inagawanywa kutokana na idadi ya watu.

Kwahiyo kama unagawa laki kwa kila mwananchi itakuwa kama hivi.

Kama nchi ina watu 1.3m itakuwa (1.3m ×100,000). Kama nchi ina watu 59m itakuwa (59m x 100,000).

Kwenye mambo ya muungano kama jeshi, polisi hayahusiki sababu hayo ni ya kimuungano.

Kunakuwa na uhuru wa kuishi, kufanya kazi, biashara, kununua ardhi kugombea nafasi yoyote nchi yoyote kwenye muungano.

Tujifunze kwa Muungano wa Mataifa mengine kama Uingereza.
 
two^ hapo! Calculations zao, wakope na kuzitumia immediately, but tozo na kodi zifuatie baadaye ziwe zinafagia mauchafua yao taratibu kwa muda mrefu hadi pasafike. Umeelewa sasa?

Upuuzi mkubwa sana unaendelea kwa sasa.
 
Umepoteza muda wako bure!

Ni mada muhimu, kwa watu makini.
Tumeungana kwenye nini? Muungano ni nini? Kuungana maana yake ni nini?

Wazenji kuchukua mikopo kwa mgongo wako, utakao ulipia wewe na watoto wako.

Mikopo inachukuliwa kiholela bila tahadhari yoyote. Sababu eti nchi haiwezi kupigwa mnada majibu mepesi kwa vitu vya msingi, kwa mustakabali wa taifa, maisha yetu, future yetu na watoto wetu.
 
Mkopo usijali muda. Vigezo viwe, Return on Investment, interest rate, tunaupeleka wapi...
Kwa Serikali hakuna mpango mkubwa wenye return ya investment ya miaka 5!. Huo hautakuwa mradi wa kiwango cha serikali
 
Ni mada muhimu, kwa watu makini.
Tumeungana kwenye nini? Muungano ni nini? Kuungana maana yake ni nini...
Hakuna aliekataa kuwa ni mada muhimu lakini sisi tunatype wenzetu wanafanya!,hawawezi kukusikiliza wameshalewa!.

Ambacho hamjui tumeshakosea zamani sana halafu mnakuja kutaka kusahihisha makosa kwa kuyafuta kwa mbele too late!.

Panapostahili kurekebishwa sio matokeo ya makosa bali ni pale palipokosewa!.
 
Hakuna aliekataa kuwa ni mada muhimu lakini sisi tunatype wenzetu wanafanya!,hawawezi kukusikiliza wameshalewa!. Ambacho hamjui tumeshakosea zamani sana halafu mnakuja kutaka kusahihisha makosa kwa kuyafuta kwa mbele too late!. Panapostahili kurekebishwa sio matokeo ya makosa bali ni pale palipokosewa!.

Unapendekeza nini? tukae kimya. Tufanye nini leo, sasa hivi kulisaidia taifa letu na watoto wetu, vizazi vyetu?
 
Nimesikitiswa sana na wale wasomi wanao jaribu kuaminisha Watanzania kwamba kuna mikopo ya bank za biashara mizuri kwa serikali. Mikopo yenyewe mingi ni ya miaka 5 na riba zinakuwa 8%~10%. Hii mikopo sio mizuri kwa serikali hasa ukizingatia uwezo wetu. Serikali kwa ushauri wangu

1. Wasikope chini ya miaka 10
2. Riba ya mkopo isizidi ukuaji wa uchumi mfano Tanzania ukuaji wa uchumi ni 5%~ 7% hivyo riba iwe hapo katikati . Kama mkopo ni kwa dollar isizidi 5% kwasababu mfumuko wa bei wetu unakuaga 2% zaidi ya USA

Mwigulu acha mikopo ya riba ya juu na muda mfupi hii inaongeza payment amount za mwezi na mwaka na kusababisha pesa nyingi kwenda kwenye mikopo.

Hili bado ni muhimu

Mwigulu Nchemba
 
Back
Top Bottom