Hakuna mtandao mbovu na wenye maudhi kama Vodacom

Kweli Vodacom kwa sasa ni majanga tu, vifurushi vya internet vya ya kwako tu vilikuwa vizuri sana ila kwa sasa naona wameamua kupunguza kwa kiwango cha ajabu. Kwa hili me naona ipo haja ya kuwahama tu coz huu ni wizi mchana kweupee.
Tulio mjini acha turudi TTCL tu maana hamna namna. Wengine matumizi yetu ya data ni makubwa kuliko hata maongezi ya simu za kawaida.
Kwa hili Vodacom wamechemsha haswaa.
 
Hawa jamaa wanataka tuwakimbie serious na mm mara ya kwnz walianza kwa Gb5 kwa 2000 saiv Mb 350 kw 2000 aiseee wamenikosa ss
 
Kudadeki, Voda ni wangese sana, me mwenyewe nlkua na offer ya 200/= napata MB300, kwa 500/= nlkua napata MB800 ya kwako tu, asaiv haipo.. Wameweka madudu kama kwako ilivyo..
 
Tatizo ttcl vocha mpaka uende kariakoo..mtandao ni 4g but speed ya chura. Sijui kwan haeajiongezi watu tuhamie mazima.
 
Enzi hizo bana watu walikuwa wanasifika kwa mitandao yao, tena ukiiona namba fulani utakisikia:
VODA - aah mkulima huyo
TIGO - huyu mwanafunzi
AIRTEL - wenye pesa zao
TTCL - mabosi serikalini
Mpaka kuna wengine walivamia mitandao wasiyoimudu ilimradi kutafuta sifa tu.
Ila siku hizi hakuna hayo mambo, mtu anatumia AIRTEL kila siku analialia tu vifurushi bei.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…