Hakuna mtu mrefu wala mfupi, ni mtazamo wako tu

Hakuna mtu mrefu wala mfupi, ni mtazamo wako tu

Gaddaf i06

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2022
Posts
1,770
Reaction score
2,841
Habari,

Nimeleta mada hii makusudi kabisa, karibuni wale mnaojiita warefu, ruksa kutuma bomu lolote[emoji4]

Mimi naamini hivi: kujiona mrefu/mfupi inategemeana na mtu uliejilinganisha nae.

Huko nyuma nimesema hivi, umbo la mtu linaweza kufanya mtu aonekane mfupi (hasa watu wanene) hata kama mrefu.

Mfano; mtu akiwa mwembamba sana, hata kama kimo chake ni 4ft ataonekana mrefu!

Mwingne akiwa na urefu mfano 5.4nk alafu akawa mnene ataonekana mfupi kwa sababu ya ule unene wake.

Nimeona habari za oh mara wafupi hivi mara vile, mara wanaviburi, wachoyo, wabinafsi nk ,huu ni uongo.. Tabia haifati kimo

Mimi nina urefu wa futi 6- lakini kwasababu nina umbo kubwa naonekana wa kawaida[emoji4]
lakini ningekuwa mwembamba kwa urefu huu ningetisha sana[emoji23]

Wanaojidai na kutamba kwamba ni warefu, ndo wale wembamba kama fimbo hata awe na urefu wa kawaida tu

Sasa jipime huo urefu wako, kama una futi 6.1+ basi wewe mrefu!
 
Back
Top Bottom