Hakuna mwanachama yeyote anayeweza kumkataa Haji Manara Yanga vinginevyo umechagua kuikataa GSM

Hakuna mwanachama yeyote anayeweza kumkataa Haji Manara Yanga vinginevyo umechagua kuikataa GSM

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Kaeni mkijua nyie utopolo kuwa Haji Manara hayupo Yanga kwa ajili ya mapenzi ya timu hiyo, yeye yuko Yanga kwa ajili ya GSM.

GSM ndio inamlipa mshahara Yanga na mwenyewe amesema live kuwa ameongezewa mshahara hata wakati ule alipokuwa amefungiwa.

Yeye Manara ni mtu muhimu sana ndani ya klabu ya Yanga, yeye ndio amefanikisha Simba kusambaratika vipande vipande na kuiachia Yanga itambe sasa hivi.

Yeye ndio anauza silaha zote za Simba pale Yanga.GSM hawawezi kumtenga Manara kwa sababu wanaamini soka la Tanzania ukiimaliza Simba ama ukiimaliza Yanga umemaliza.Yeye ana connections na watu wa Simba ambao wana njaa.Manara akipewa fungu basi anajua kule upande wa pili amshike nani ili watambe.

Kuna mamluki kibao ndani ya mnyama ambao wanafanya kazi na kiumbe huyo kutokana na njaa na ulofa.
Ally Kamwe amefanikiwa kuimudu nafasi ya usemaji ndani ya Yanga lakini Manara ni muhimu sio kwa domo lake hapana, umuhimu wake uko kwenye mipango ya kuivuruga klabu aliyokuwa akiisema zamani.

Kule alikokuwa zamani alikuwa anajua vyoteeee, walimuingiza hadi jikoni wakijua hawezi kwenda upande wa pili kutokana na mapenzi na kauli zake za nyuma akiwa na timu hiyo kuwa hawezi kwenda upande wa pili.
Kwa sasa Simba wana kazi kubwa sana kuisumbua Yanga kwa sababu ya huyo kiumbe, kiumbe huyo anapewa siri zote za wekundu wa msimbazi na anazipeleka hapo jangwani.

Hivyo basi kama akitokea mwanachama au shabiki anapinga uwepo wa Manara pale jangwani ajue kuwa anapinga udhamini wa GSM.

Ukimuondoa Magoma Shaaban, hakuna mjanja yeyote ndani ya Yanga anayeweza kusimama hadharani akasema Manara hapana, Kamwe anatosha.Hayupo na hatokuwepo.

Hivi Manara kwa Press ya leo kipi hasa alichokifanya ambacho Kamwe hajakifanya? Basi tarehe 4 watu wakijaa uwanjani atadai yeye ndio kajaza uwanja.Ujinga mtupu.

Njia pekee ya Simba kumfukuzisha Manara pale Yanga ni kuhakikisha mipango yao haijulikani na watu wengi kama wanavyofanya wenzetu pale Avic.

Kama Simba ataendelea kuburuzwa na Yanga basi Manara ataendelea kupeta na kumharibia kibarua kijana Ally Kamwe ambaye mimi pamoja na usimba wangu anaongea vizuri, licha ya utani wake lakini hana ugomvi na Mashine ya Kuongea Ahmed Ally.Ni maswahiba na wanaongea kishkaji sana ukilinganisha na kiumbe huyo wa Zaylisa.

Narudia hakuna mtu wa kumfukuzisha Manara kazi pale Yanga zaidi ya GSM wenyewe, hakuna na hayupooooo.Kama mnataka njaa irudi basi muondoeni.Magoma Shaaban pekee ndio anaweza.
 
Back
Top Bottom