SoC01 Hakuna Mwanafunzi asiye na uwezo wa kitaaluma ni mipango tu na kujiamini

SoC01 Hakuna Mwanafunzi asiye na uwezo wa kitaaluma ni mipango tu na kujiamini

Stories of Change - 2021 Competition

DustBin

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2021
Posts
609
Reaction score
604
Kama mwanafunzi hana utindio wa ubongo huyo anafundishika na akafanya vizuri kabisa katika masomo yake.

Wanafunzi wamegawanyika katika makundi makuu matatu;-

  1. Ni wanafunzi ambao wana uwezo mkubwa wa uelewa na kutafakari; hawa wakifundishwa kidogo tu inawatosha.
  2. Na wengine wapo wenye uwezo wa katikati ambao wanatakiwa waongezewe njia zilizoboreshwa za ziada za ufundishwaji, pamoja na juhudi zao binafsi ndio wanaelewa.
  3. Na kundi la mwishoni la wale wanaosemwa kuwa hawana akili, sio kama hawana akili hapana! Isipokuwa akili zao zimelala zinahitaji kuamshwa na kuchangamshwa. Kundi hili la wanafunzi linahitaji ukaribu wa mwalimu na mbinu shirikishi za ufundishwaji. Hata hivyo wanafunzi wa aina hii wanatakiwa walazimishwe au wajilazimishe kusoma. Kwa kawaida anayetaka kufunguliwa mlango hana budi agonge kwa kadiri anavyoweza, kama ndani ya nyumba kutakua na watu watamfungulia tu iwe kwa kuridhia au kwa kuchoshwa na kelele za kugongwa kwa mlango, lakini lazima atafunguliwa. Vivyo hivyo wanafunzi wa kundi la tatu wanatakiwa walazimishe kusoma, hadi hapo taaluma yenyewe itakapokubali kukita kwenye mbongo zao.
Kwenye hili nina mifano ya kutosha; wakati nipo sekondari kuna mwanafunzi hakuwa na uwezo wa hivyo lakini mwenyewe alijibidiisha sana katika kusoma na alikua mfuatiliaji wa masomo yake kiasi walimu wa masomo hayo wakampenda, sio kwa sababu anafanya vizuri la hasha! Kwa kuwa tu alikua mfuatiliaji na anayapenda yale masomo, hili lilimsaidia kuongeza uwezo wake wa kitaaluma hatimaye hakufeli kwenye mtihani wa mwisho.

Hivyo mwanafunzi anatakiwa ajitambue kwanza yeye yupo katika kundi gani? Kisha ndio aanze kujipanga kulingana na kundi alilopo. Hata hivyo kusoma sana kuna faida kubwa sana hasa kwa wanafunzi wa kundi la tatu ambao wanahitajika kutumia muda mrefu sana katika kusoma na kukariri masomo.

Ingawa kuelewa na kukariri ni vitu viwili tofauti, lakini kukariri kuna msaada mkubwa katika kuelewa masomo hasa katika masomo yasiyoeleweka kwa haraka kama masomo ya sayansi na hisabati. Hivyo wanafunzi wasibweteke na wasiige wenzao kwani hawajui hao wanaowaiga wapo katika kundi gani katika makundi haya matatu ya uelewa wa wanafunzi. Mwanafunzi wa kundi la pili akimuiga mwanafunzi wa kundi la kwanza hawezi kufanya vizuri katika masomo yake.

Mwenzie akishasoma ubaoni mara moja na mwalimu hana haja ya kusoma tena anakua ameshaelewa hivyo utamuona haangaiki kujisomea. Sasa huyu ukimuiga na wewe ukawa hujisomei kama yeye utafeli, wewe wa kundi la pili unahitaji muda wa ziada kujisomea na kurejea masomo yako.

HITIMISHO

Jambo la msingi ni kwamba hakuna mwanafunzi asiye elewa, au hakuna mwanafunzi asiye na akili; wanafunzi wote wana akili na wanaelewa wakisomeshwa vizuri. Wanacho tofautiana ni viwango vya uelewa. Hivyo wewe mwanafunzi ambaye uwezo wako wa uelewa ni mdogo usivunjike moyo, unatakiwa kujiongeza zaidi na kujibidiisha na kujilazimisha kusoma mara kwa mara na utumie muda mrefu katika kusoma mwisho wa siku utaona mwenyewe namna masomo yatakavyo kukumbatia mpaka mwenyewe utajishangaa.

Shime kwa wazazi ambao wamejishukuru na kusema “mimi mwanangu hata hana akili, anakua wa mwisho” msiwavunje nyoyo watoto wenu, mnatakiwa kuwapa motisha na kuwajenga kifikra kwamba wanaweza kama watatoa juhudi za dhati katika masomo yao. Na nyie wazazi muwasimamie wakiwa nyumbani muda wao mwingi wautumie katika kusoma. Lengo lisiwe kuwa wa kwanza darasani, lengo ni kujiondoa katika kundi la wenyekufeli. Kuwa wa kwanza darasani ni matokeo tu leo anaweza kuwa huyu kesho akawa mwingine. Hata hivyo kuwa wa kwanza darasani sio kigezo cha kuwa na uwezo mkubwa kushinda wengine.

DustBin
 
Upvote 1
Back
Top Bottom