hakuna mwanangu atakaekanyanga shule za serikali

achana na upande wa tatu,naomba uniambie maana ya kukufuru ili tuendelee

Naona una ustaarabu lakini uliamua kujitoa kwa makusudi. Unapobeza watoto wa wenzako wanao soma shule za kata na zinginezo zilizo na inferior standards kisa tu mwenyezi Mungu kakujalia uwezo (at least kwa sasa) huko ni kukufuru baraka alizokupatia mwenyezi Mungu. Na hapa ndipo msingi wa hoja yangu ulipolala, kwamba hata ambao hawajapewa uwezo sio wote wamelala. Wapo wengi tu ni wapiganaji lakini they are unfortunate. Kwanini they are unfortunates? God knows!
 

katika maisha yangu yote sijawahi kumbeza mtu kwa sababu kasoma shule za serikali ama hizi za juzi juzi za kata, na hapa jamii forum sijawahi kumbeza mtu,unaweza kuonyesha ni wapi nimembeza mtu kwa sababu kasoma shule ya kata?fanya hivyo tena naomba uni quote na u-highlight kwa rangi nyekundu ili kila mtu aone.

umechanganya ndugu yangu hata kabla hujanipa majibu. mimi siku zote nabeza shule zote za serikali lakini si wanafunzi wanaosoma hizo shule kwa sababu ni mbovu hata ukiziacha hizi za kata hakuna shule yoyote nzuri ya serikali. na nimekuwa nikisema muda wote kuwa hizi sio shule bali vituo vya kufanyia mitihani na hata mimi niliwahi kufanyia mitihani katika vituo hivyo lakini sikuwahi kusoma maana sikufundishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…