Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
HAKUNA NABII NA MTUMISHI WA MUNGU ALIYEJIINGIZA KWENYE SIASA AKASHINDA PASIPO KUWA MPIGANAJI WA VITA. MANABII WENGI WALIOINGIA KWENYE SIASA WALIUAWA KWA SABABU HAWAKUWA WARRIOR
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Hii ni angalizo kwa wale Watumishi wa Mungu, Manabii na mitume wa wakati huu ambao mnaona mnawito WA kiutumishi kama Mungu.
Usitumie unabii au utume wako bila kufahamu matokeo yake unapojiingiza kwenye baadhi ya ishu kama kujiingiza kwenye Siasa na kukosoa Wanasiasa na Watawala.
Ukisikia Nabii au Mtume au mtumishi wa Mungu aliyeuwa kwenye Kisa chochote kile tambua Mhusika huyo hakuwa na mafunzo ya kivita, kijeshi yaani hakuwa Warrior, shujaa wa vita.
Hii inamaanisha kuwa, Kuwa Nabii au Mtume pekee yake haitoshi kujilinda katika Kazi yako ya utume. Ni lazima uwe na sifa za Ziada kulingana na Kazi utakazotumwa.
Endapo ikatokea huna sifa za Ziada kama upiganaji, mafunzo ya KIJESHI na ukomandoo hii itamanisha umejiweka katika nafasi mbaya ya kuangamizwa mapema zaidi kabla ya Muda wako.
Utakamatwa utafungwa, utateswa na wakati mwingine na mara nyingi utauawa.
Ndipo Ile Aya ya kwenye Torati inayosema "Uwe Hodari na ushujaa mwingi" inapofanya Kazi. Yaani uwe Jasiri lakini pia uwe na mafunzo ya kijeshi na kivita .
Sio uwe tuu Unajiamini alafu huna ujualo kwenye uwanja wa mapambano. Ukiagiziwa tuu wasiojulikana hata watatu kinyume na taratibu unakamatwa kama Kuku mwenye kideri.
Wewe uliona wapi Warrior akakamatwa kizembezembe? Uliona wapi!
Mungu humuokoa anayeweza kujiokoa.
Kuwa kwako muombaji au Mwaminifu haimfanyi Mungu afanye wajibu wako wa kujilinda Kimwili na kupigana kwa mapigo ha Kimwili
Mungu ana amplifier kile ulichonacho.
Orodha wa Watumishi wa Mungu waliouawa wengi wao walikuwa wazembe kwenye kujilinda.
Mfano wanafunzi karibia wote wa Yesu yaani mitume 10 waliuawa kwa Sababu hawakuwa Warrior.
Yesu mwenyewe aliuawa kwa Sababu hakuwa Warrior.
Kiutawala hata uwe na miujiza ya kushusha Moto kutoka Mbinguni, Kufufua Wafu n.k. Kama wewe sio Warrior IPO siku utakamatwa na kuuawa na Mashujaa wenye kujua kuchezea silaha na kupigana.
Labda usijihusishe na Siasa
Au usiwe mtumishi unayejihusisha na mambo ya utetezi wa Haki. Yaani usiwe mtetezi wa Haki kupita Kiasi.
Ibrahim alikuwa Warrior, alipokamatwa na Mfalme Nimrodi akatoroka kimazabe kama mjuavyo majasusi siku zote wanaakili nyingi Nje ya mapambano ya kivita. Ibrahim alizeeka baada ya mapambano Mengi katika ujana wake.
Huyo ni Legend.
Musa alikuwa Warrior tena aliyefunzwa katika Jumba la Kifalme la Farao.
Alikuja akatoroka baada ya serikali ya Farao kutoa tamko la kutaka Musa akamatwe kwa kuua Mmisri. Musa akakimbilia nchi ya Kush. Huko nako akakinukisha Mpaka akaja kuwa Mfalme kwa Miaka zaidi ya 18. Kisha akatoroka tena akakimbilia Midiani.
Musa pia alizeeka Akiwa ameshiba siku nyingi tuu. Huyo ni Legend
Daudi Alikuwa Warrior, serikali ya Mfalme Sauli ilimsaka mchana na usiku ili kumuua kwa zaidi ya Miaka 12 Jamaa anakimbia huku na huko huku akipigana na majeshi ya serikali. Na kila mara alipopata Nafasi ya kumuua Mfalme Sauli yaani Uso kwa Uso alimsamehe.
Daudi ndiye alimuua Goliath(shujaa wa wakati wote wa Wafilisti).
Nataka kusema nini?
Kutenda Wema Sana, kuomba Sana na kuwa mtumishi wa Mungu kikamilifu haitoshi kujiingiza kwenye kupambana na Serikali kwa kile unachokiita kutetea HAKI za watu au kutetea Haki Fulani.
Kila Jambo Lina Kanuni zake.
Serikali inaweza kukufanya chochote na huyo Mungu asifanye lolote lile.
Ushaambiwa Mungu hawi radhi na watu wapumbavu.
Kama Ibrahim na Musa wenye Imani na walioomba Mungu walikuwa warrior, mambo ya Kimwili waliyaendesha Kimwili wakimshirikisha Mungu. Kwa nini wewe mtumishi wa Mungu ujiingize kwenye kutetea HAKI kichwakichwa ukitegemea tuu maombi badala ya kujifunza pia na ushujaa mwingine WA Kimwili.
Nafahamu wengi wanamfuata Yesu ambaye ndiye Master Wao.
Lakini iko hivi kama alivyo Mwalimu/Master ndivyo walivyo wanafunzi wake.
Muangalie alichofanyiwa Yesu kisha angalia Wanafunzi wake.
Kisha muangalie Musa alivyoshinda kisha muangalie Mwanafunzi wake aitwaye Joshua. Yaani kinatoka chuma kinaingia Chuma.
Muangalie Daudi, kisha muangalie Suleiman.
Muangalie Ibrahim kisha muangalie Isaka.
Huwezi mtegemea Master akusaidie kwenye Jambo ambalo yeye mwenyewe lilimshinda. Hilo hata mtoto mdogo anajua fika.
Achana na hadithi za Paulo na Sila Gerezani. Tunaangalia mwisho wao nini kilitokea.
Unapotaka kutumia principles za mtu Fulani ili awe master wako katika Jambo Fulani angalia huyo master wako kwenye Jambo hilo alifanikiwa kwa hizo principles zake.
Sijasema watu wasimfuate Yesu. Nope!
Ila nazungumzia kamwe usije tumia principles za Yesu katika kutetea HAKI za watu na kujiingiza kwenye Siasa. Utapigwa mapema Sana na hakuna lolote litatokea na watesi wako watazidi kupeta na kufanikiwa.
Mtumie Yesu kwenye Masuala ya Kiroho zaidi na kufanya miujiza sijui kuponya watu Magonjwa, kuwatia moyo Watu, kuwafunisha mambo ya Msamaha.
Lakini kamwe usimtumie Yesu kwenye Masuala ya Kisiasa na kiutawala huko principles zake hazifanyi Kazi Kabisa na wengi waliojaribu waliangukia Pua.
Kisiasa adui yako huwezi kumwombea.
Kisiasa kuna Muda lazima mtu ujiongoze mwenyewe hasa kwenye Hatari.
Wewe badala ukimbie ukajihami ujifiche wewe unasubiria ukamatwe. Akili za wapi hizo.
Kijeshi na Warrior wanajua nini chakufanya katika mambo hayo.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam